Na Mwandishi Maalum
New York
Imeelezwa kwamba baadhi ya nchi zitashindwa kutekeleza kwa kasi matarajio na matumaini makubwa waliyonayo vijana.
Matarajio na matumaini hayo ni yale yanayoletwa na utandawazi na matumizi mkubwa ya vyombo vya habari vya kijamii.
Tahadhari hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue.Alikuwa akizungumza katika Mkutano wa kilele wa Vijana uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Amesema utandawazi ambao unaendeshwa na teknolojia unawafanya vijana kuwa katika kijiji kimoja cha kimataifa. Na kuwajengea ufahamu mkubwa wa wapi walipo au wapi wanatakiwa kwenda.
Balozi Sefue akaeleza , Utandawazi huo umewajengea vijana matumaini makubwa ya kisiasa, kiuchumi , kiutamaduni na kijamii.“ Lakini, baadhi ya matarajio hayo hayawezi kutekelezwa na serikali nyingi kupitia raslimali zilizonazo au sera zilizopo na kwa kasi wanayoitaka vijana”.
“ kwa maneno mengine, ingawa Utandawazi unawapa matarajio kwa vijana wetu, lakini siku zote utandawazi huohuo hautoi nyenzo sahihi za kuwapatia uwezo na fursa vijana ya kutimiza ndoto zao”.akasisitiza Balozi Sefue.
Akatahadharisha kuwa kutotimizwa kwa ndoto hizo za vijana, kunaweza kusababisha madhara makubwa. Madhara ambayo yanaweza kuvuka mipaka ya nchi.
Kwa hiyo akasema, ni muhimu kuunga mkono juhudi za serikali za kitaifa na kikanda, za kuujenga uutandawazi wa haki utakao wawezesha vijana siyo tu kuwa na matumaini bali pia kuwa na fursa ya kumiliki mali.
Kuhusu matumizi ya vyombo vya habari vya kijamii ambayo vijana wengi wanajitanabaisha navyo, Balozi Sefue amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, ingawa vyombo hivyo ni nyezo muhimu katika kuleta mabadiliko chanya. Kwa bahati mbaya vyombo hivyo kama havitatumia ipasavyho vinaweza pia kuleta matokeo mabaya.
Mwakilishi huyo wa Tanzania katika UM, akabainisha kuwa serikali yake inaamini kwamba vijana siyo tu viongozi wa kesho, kwani wanaweza kuwa viongozi wa leo na kutoa mchango mkubwa wa kulijenga taifa lao kwa kushirikiana na wazee wao.
Akasema kwa kutambua umuhimu wa ushiriki wa vijana katika ujenzi wa nchi yao, ndio maana serikali ya Tanzania imepitisha sera zinazo wawezesha vijana wa kike na kiume kupata nafasi za uongozi katika vyombo vya utoaji wa maamuzi likiwamo Bunge.
Mkutano huo ambao ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, uliwashirikisha mawaziri wanaohusika na masuala ya vijana kutoka nchi wanachama wa UM. Pamoja na mambo mengine ulijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana duniani kote na namna ya kuzitafutia ufumbuzi.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali duniani. Pamoja na wawakilishi kutoka taasisi zisizo za kiserikali. Na ulitoa na maazimio mbalimbali yakiwamo ya kubuni mbinu mbadala za kushughulikia matatizo ya vijana zikiwamo ajira.
Thanks for utandawazi, I think vijana wa leo know very well what there government is capable of doing for them given the available resources. The main problem is the corrupt governments are being exposed of their shameless acts through utandawazi and claim they don't have resources to deliver basic needs, this is what vijana will not accept and will hold the governments accountable. As kijana I'm offended by this and urge other vijana not to accept this bs, utandawazi is here to stay, nothing will change it, this is information age, you're either with it or stay out of it. Arabian (Tunisia and Egypt) style revolution will soon spread to the rest of Africa is leadership don't get their act together.
ReplyDelete