Mjasilia mali huyu ambaye jina lake halikuweza fahamika mara moja akiwa maebeba nyama ambayo alikuwa akiipeleka buchani kwake wakati alipokuwa akitokea machinjioni leo maeneo ya barabara ya Jamhuri,mjini Dodoma kama alivyonaswa na mpiga picha wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2011

    Hii ni hatari sana, na hivi ndivyo ilivyo nchi nzima. Yaani nyama ikiwa inapelekwa buchani ni lazima iwe ni suala la kuonekana kwa jamii nzima na uwezekano ni mkubwa sana kuwa itaathiriwa na vijidudu hatarishi kwa afya za walaji. Buchani nako inakaa wazi siku nzima na hata siku zinazofuatia. Hivi manispaa za miji husika hamlioni hilo??? Leo hii mimi nina umri wa zaidi ya miaka 30, lakini tokea enzi za uvulana wangu nimekuwa nikishuhudia utaratibu huu huu. Hamjifunzi na kufikiri????? Manispaa moja ijitokeze na kuwa mfano wa kuigwa kwa zingize, ubunifu na kujituma katika kuleta mabadiliko vinahitajika jamani, mambo haya ni ya kizamani na ni hatari.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2011

    hapo HACCP vipi watu wa nutrition na food sc.?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2011

    kuna mambo ambayo yako mikonono mwetu ila bado tunadhihirishia dunia kwamba sisi bado tunahitaji kutawaliwa na kupigwa viboko tu ukiangalia ni mambo mengi mnooo hayana hesabu.kwa mfano swala la usafi wa mazingira tunayoishi hauhitaki digriii ila sisi waafrika sijui.tofauti sana na waafrika wa Rwanda kwani wale wana asili ya usafi kwa kweli ukipita pale utadhani si afrika.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2011

    Mimi huwa naona ka-gari fulani hata jijini Dar, kachafuu kanasambaza nyama maeneo kadhaa, nyama hiyo ikiingia buchani nako inakaa nzi kibao wanaanza kuishambulia, hadi mnunuzi unapokuja kununua, unakuwa unanunua na wadudu, usipoenda kuipika vema hiyo nyama, unaweza ukaharisha hadi ukakoma!. Tanzania nzima ina shida kubwa. Waheshimiwa, watu wa chakula wekeni sera wazi za namna ya utunzaji vitu kama nyama na vyakula vingine ambavyo ni fresh. Kuna yale mafriji makubwa yenye vioo kama supermarket kama yale ya mlimani city, kwa nini mabadiliko Tanzania yanachukua miongo mingi sana kutokea? Watu wa chakula, mabwana afya acheni rushwa tekelezeni kazi zenu, mamlaka husika chukueni hatua, mkichukua hatua tabia za wenye mabucha zitabadilika watajifunza namna ya kutunza vyakula "raw" kama nyama n.k.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 28, 2011

    UZURI WA BONGO HAKUNA SOIL BACTERIA. IMEPITISHWA NA WIZARA YA AFYA HIYOO

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2011

    Nimekula hiyo nyama miaka 40 na kiko fit kinoma! Acheni mambo ya ughaibuni, nzi waking'ong'a nio nyama inazidi utamu. Hiyo nyama ni organic na ughaibuni ni bei mbaya!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 29, 2011

    Heri hii kuliko samaki wa sumu toka Japani

    ReplyDelete
  8. sasa Hizo BUTI NYEUPE alizovaa mpaka barabarani si za kuvalia kule machinjioni na kuziacha huko ili nyama isipate wadudu?

    Sasa amezikanyagia nje/chini halafu baadae anarudi nazo tena machinjioni akiwa ameshabeba wadudu halafu anawaingiza humo machinioni.

    Kaazi kwel kwel

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...