Home
Unlabelled
Nyama ikipelekwa buchani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hii ni hatari sana, na hivi ndivyo ilivyo nchi nzima. Yaani nyama ikiwa inapelekwa buchani ni lazima iwe ni suala la kuonekana kwa jamii nzima na uwezekano ni mkubwa sana kuwa itaathiriwa na vijidudu hatarishi kwa afya za walaji. Buchani nako inakaa wazi siku nzima na hata siku zinazofuatia. Hivi manispaa za miji husika hamlioni hilo??? Leo hii mimi nina umri wa zaidi ya miaka 30, lakini tokea enzi za uvulana wangu nimekuwa nikishuhudia utaratibu huu huu. Hamjifunzi na kufikiri????? Manispaa moja ijitokeze na kuwa mfano wa kuigwa kwa zingize, ubunifu na kujituma katika kuleta mabadiliko vinahitajika jamani, mambo haya ni ya kizamani na ni hatari.
ReplyDeletehapo HACCP vipi watu wa nutrition na food sc.?
ReplyDeletekuna mambo ambayo yako mikonono mwetu ila bado tunadhihirishia dunia kwamba sisi bado tunahitaji kutawaliwa na kupigwa viboko tu ukiangalia ni mambo mengi mnooo hayana hesabu.kwa mfano swala la usafi wa mazingira tunayoishi hauhitaki digriii ila sisi waafrika sijui.tofauti sana na waafrika wa Rwanda kwani wale wana asili ya usafi kwa kweli ukipita pale utadhani si afrika.
ReplyDeleteMimi huwa naona ka-gari fulani hata jijini Dar, kachafuu kanasambaza nyama maeneo kadhaa, nyama hiyo ikiingia buchani nako inakaa nzi kibao wanaanza kuishambulia, hadi mnunuzi unapokuja kununua, unakuwa unanunua na wadudu, usipoenda kuipika vema hiyo nyama, unaweza ukaharisha hadi ukakoma!. Tanzania nzima ina shida kubwa. Waheshimiwa, watu wa chakula wekeni sera wazi za namna ya utunzaji vitu kama nyama na vyakula vingine ambavyo ni fresh. Kuna yale mafriji makubwa yenye vioo kama supermarket kama yale ya mlimani city, kwa nini mabadiliko Tanzania yanachukua miongo mingi sana kutokea? Watu wa chakula, mabwana afya acheni rushwa tekelezeni kazi zenu, mamlaka husika chukueni hatua, mkichukua hatua tabia za wenye mabucha zitabadilika watajifunza namna ya kutunza vyakula "raw" kama nyama n.k.
ReplyDeleteUZURI WA BONGO HAKUNA SOIL BACTERIA. IMEPITISHWA NA WIZARA YA AFYA HIYOO
ReplyDeleteNimekula hiyo nyama miaka 40 na kiko fit kinoma! Acheni mambo ya ughaibuni, nzi waking'ong'a nio nyama inazidi utamu. Hiyo nyama ni organic na ughaibuni ni bei mbaya!
ReplyDeleteHeri hii kuliko samaki wa sumu toka Japani
ReplyDeletesasa Hizo BUTI NYEUPE alizovaa mpaka barabarani si za kuvalia kule machinjioni na kuziacha huko ili nyama isipate wadudu?
ReplyDeleteSasa amezikanyagia nje/chini halafu baadae anarudi nazo tena machinjioni akiwa ameshabeba wadudu halafu anawaingiza humo machinioni.
Kaazi kwel kwel