Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Muhidin Maalim Gurumo akishukuru kwa michango aliyopata wakati wa onesho maalum la kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu yake lililofanyika Jumamosi usiku ukumbi wa Mango Garden jijini Dar.Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akimkabidhi Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Muhudin Gurumo, fedha zilizochangwa na wadau wa muzikiKiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Muhidin Gurumo (katikati) akiwa kazonngwa na mashabiki wakati akiwaongoza waimbaji wa bendi hiyo katika onesho hilo maalum la kuchangisha fedha
Onyesho hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo lilifanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden, ulioko Kinondoni jijini Dar es Salaam, lilipokelewa vema na wapenzi na wadau wa muziki kwa ujumla ambao walichangia fedha za kutunisha mfuko wa kumsaidia mwanamuziki huyo.
Akizungumza katika uzinduzi wa harambee hiyo, mgeni rasmi Naibu Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge, alianza kwa kumshukuru na kumpongeza mratibu wa tamasha hilo Asha Baraka na bendi nzima ya Twanga Pepeta kwa kuona thamani ya mwanamuziki huyo.
“Kabla ya yote nichukue fursa hii kumshukuru na kumpongeza Asha Baraka na bendi nzima ya Twanga Pepeta kwa uamuzi wao wa kuandaa onyesho maalum la kumchangia mzee wetu, Muhidin Gurumo, ambaye amestaafu muziki kwa sababu ya maradhi,” alisema Songoro na kuongeza:
“Wakati nikiongea naye mzee Gurumo ameniambia kuwa alianza muziki mwishoni mwa 1950 na kufikia mwaka 1961 wakati nchi yetu ikipata Uhuru tayari alikuwa mwimbaji, huu ni muda mrefu kweli, leo tunapozungumza ana miaka 71 na alikuwa bado anaimba kama sio maradhi,” alisema na kushangiliwa.
Alisema wanamuziki hawana malipo ya uzeeni, basi kitendo kilichofanywa na Asha kinastahili kupongezwa na kuigwa na wadau wa muziki na wana jamii kwa ujumla kwa sababu fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo zitamsaidia sana mlengwa katika maisha yake mapya nje ya muziki. Picha na Habari na Francis Dande
Kiongozi wa Msondo Ngoma Muhidin Maalim Gurumo akiwa na kiongozi mwenzie Said Mabera
Naibu Meya wa Kinondoni mhe. Songoro Mnyonge akiongea kwenye onesho hilo huku Asha Baraka akiwa pembeni yake.ONESHO maalum lililoandaliwa na Mkurugenzi wa African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka, la kuchangisha fedha kwa ajili ya kumpatia kiongozi wa Msondo Ngoma, Muhidin Gurumo, aliyelazimika kujistaafisha muziki kutokana na kuumwa, lilifana.
Onyesho hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo lilifanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden, ulioko Kinondoni jijini Dar es Salaam, lilipokelewa vema na wapenzi na wadau wa muziki kwa ujumla ambao walichangia fedha za kutunisha mfuko wa kumsaidia mwanamuziki huyo.
Akizungumza katika uzinduzi wa harambee hiyo, mgeni rasmi Naibu Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge, alianza kwa kumshukuru na kumpongeza mratibu wa tamasha hilo Asha Baraka na bendi nzima ya Twanga Pepeta kwa kuona thamani ya mwanamuziki huyo.
“Kabla ya yote nichukue fursa hii kumshukuru na kumpongeza Asha Baraka na bendi nzima ya Twanga Pepeta kwa uamuzi wao wa kuandaa onyesho maalum la kumchangia mzee wetu, Muhidin Gurumo, ambaye amestaafu muziki kwa sababu ya maradhi,” alisema Songoro na kuongeza:
“Wakati nikiongea naye mzee Gurumo ameniambia kuwa alianza muziki mwishoni mwa 1950 na kufikia mwaka 1961 wakati nchi yetu ikipata Uhuru tayari alikuwa mwimbaji, huu ni muda mrefu kweli, leo tunapozungumza ana miaka 71 na alikuwa bado anaimba kama sio maradhi,” alisema na kushangiliwa.
Alisema wanamuziki hawana malipo ya uzeeni, basi kitendo kilichofanywa na Asha kinastahili kupongezwa na kuigwa na wadau wa muziki na wana jamii kwa ujumla kwa sababu fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo zitamsaidia sana mlengwa katika maisha yake mapya nje ya muziki. Picha na Habari na Francis Dande
Michuzi.. nimeangalia katika habari hii sijaona imeelezwa kuwa Guromo anahitaji kiasi gani kwa matibabu na kiasi gani kimechangwa.. hebu fuatilia na tuliweke wazi kwa wadau..
ReplyDeleteHarambe hii aliyoibuni Dada Asha Baraka ni ya Kishujaa tena,mwanamama huyu ni Shujaa,anajali thamani ya ubinadamu,hila tuna ombi moja kuwa
ReplyDeleteDada Asha Baraka,aunde kamati na kufungua akaunti ya benki ,hili wadau walio nje na ndani ya nchi waweze kutoa michango yao.
wadau
FFU aka Ngoma Africa band
MUHIMU SANA SANA ASHA BARAKA AMEONYESHA NJIA, hebu hili litangazwe kupitia media mbalimbali maana NAAMINI WATU WENGI SANA WATACHANGIA WALAU KUMGARIJI MZEE WETU SHUJAA.. AMEIMBA KWA MUDA MREFU SANA HADI UMRI HUU (71yrs).. Account iwe wazi itangazwe na WATU WATACHANGIA NAAMINI HIVYO
ReplyDelete"Ni kweli bendi ya African Stars "twanga pepeta" imeonyesha njia katika kusaidia wasanii wenzao. tuwaunge mkono kwa kumchangia zaidi huyu mzee mkongwe ambaye ni mfano wa kuigwa na wasanii wengine.
ReplyDeleteHongera mama Asha Baraka
ReplyDelete