Mh. Pinda
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ana siri nzito kuhusu hatima ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Jairo baada ya jana kusema kuwa Rais Jakaya Kikwete amempa maelekezo mapya kuhusu suala hilo.Pinda alisema hayo, baada ya gazeti la Mwananchi kumtaka aeleze hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi ya katibu mkuu huyo aliyetuhumiwa juzi bungeni kuwa aliziagiza zaidi ya taasisi 20 kuchanga Sh50milioni kila moja kwa ajili ya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake.

Dkt. Hosea
"Suala hilo bado tunalifanyia kazi," alisema Pinda alipotakiwa kueleza maagizo aliyopewa na Rais baada ya kuwasiliana naye juzi na jana. "Ndio niliwasiliana naye lakini, ametoa maelekezo mapya kuhusu suala hilo ambayo tunalazimika kuyafanyia kazi kwanza."

Akizungumzia suala hilo la Jairo bungeni juzi, Pinda alisema: "Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana. 
Mh. Shellukindo

Bw. Jairo
Mh. Ngeleja
 Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua."Tuhuma za rushwa katika Wizara ya Nishati na Madini ziliibuliwa juzi na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo alipokuwa akichangia Makadirio ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni juzi.

Shellukindo alisema, Jairo aliziandikia barua idara na taasisi hizo akiziagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma."Tena inaagiza kwamba fedha hizo zikishatumwa kwenye akaunti hiyo, wizara ipewe taarifa kupitia Ofisi ya DP kwa ajili ya utaratibu," alisema Shellukindo akiinukuu barua hiyo.

Habari kamili nenda Mwananchi
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2011

    Huu ni mchezo wa kuigiza,tushachoka blablaa,sioni wa kuadabishwa hapa,hii tabia ni ya viongozi wa wizara zote kwa muda wote wanapokuwa bungeni ,sio kama ni kitu kipya.Lakini leo ndio kimejulikana waziwazi,angalau mungu ametuonyesha wanayotufanyia kila wakikutana kwenye bunge,viongozi tuliowachagua wanapeana hongo kugushi matumizi ya wizara zao na kunyonya pesa ya walipa kodi.
    Inauma sana,lakini najua hili litakwisha kinyemela na hakuna hata atakae wajibika,Bongo tambarare!
    Kwa staili hii tutabakia kukamata wauza cd feki za nyimbo za injili,machinga,mama ntilie nk nk

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2011

    Takukuru wanafanya nini wakati bomu lishalipuka ?hii ni kesi ya polisi tu,maana ushahidi upo na akaunti ipo,wahusika wote wafilisiwe mali zao maana hawakuzipata kihalali.
    Takukuru walitakiwa wao ndio wagundue hii njama na sio vinginevyo.
    Tumechoka na hizi tabia mpaka mwenyezi mungu atuangamize na mabalaa ndio tutakoma.
    Kwani wangapi wameondoka(mauti) na kuacha mali na pesa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2011

    Acheni siasa jamani. barua mbona inajieleza vizuri tu. Fedha za kuchangia gharama kwa sababu viongozi waandamizi na maafisa mbalimbali watakuwa huko kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali. Mnafikiri wakienda huko wanalipwa hewa? Wanahitaji perdiem hao. Si pesa zinatakiwa? Mnakurupuka tu bila kutafakari. Fedha zimepelekwa kwenye akaunti ya GST kwa sababu hawawezi kubeba cash kwa hiyo ni lazima kuwe na bank transfer kwenda kwenye taasisi ambayo inahusika na hiyo bajeti. Na naamini GST iko chini ya hiyo wizara. Wanasiasa msiwaendekeze, wanaharibu maisha ya watu hao.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 20, 2011

    Hii kesi ipo wazi,kama taasisi 20 zilitakiwa kuchanga mil. 50 ea,tayari kuna taasisi zilizokwisha deposite pesa kwenye akaunti hiyo,kwa maana wamechangia kutoa rushwa.
    Naomba hili zoezi lifanywe kwa bajeti za wizara zote,tuone kama huu mchezo ndio uliotumika.
    Kila idara iliyokubali kutoa pesa nayo ipo hatiani,wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria, period.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 20, 2011

    We anony wa tatu wa July 20 09:19am kama husomi habari na huelewi mambo yaendavyo usiandike bila kujua undani wa unachoandika, ukweli ndio huu hapo chini kutoka bungeni:

    MAELEZO YA MBUNGE FULANI: “Aondoke huyo!” (source IPP)

    “Mheshimiwa Spika, sasa hizi fedha zote shilingi 50 milioni kwa kila taasisi na kila idara ni shilingi ngapi? Nimefanya utafiti nimegundua hizo fedha nadhani zinazidi shilingi bilioni moja, zimekwenda wapi? Kwa utafiti wangu wa karibu nimeuliza hizi taasisi zimekuja kwa fedha zao wamejigharimia wenyewe per diem. Kama kuna fedha zote hizi zimekwenda wapi? Waziri atuambie hizi fedha na imesainiwa, sijamaliza. Inasema; nashukuru kwa ushirikiano wako, David K. Jairo, Karibu Mkuu.

    “Mheshimiwa Spika, barua nitaiweka mezani ninayo hapa. (Makofi)”

    Baada ya Shellukindo, Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, alimtaka Waziri Mkuu kumuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), afanye ukaguzi wa dharura mahesabu ya wizara hiyo.

    Sendeka alisema anashindwa kuelewa fedha hizo zimekusudia kufanya nini na zifuatiliwe kama bado ziko katika akaunti ya NMB kama zilivyoelekezwa ama tayari zimechakachuliwa.

    NIPASHE ilipomuuliza Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, kuhusiana na kashfa hiyo, alijibu kwa kifupi “No comments” (sina la kusema).

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 20, 2011

    we anonymous wa wed jul 20, 09:19:00 AM 2011 una umri gani wewe hasa? umesikia wapi kuwa gharama za usafir wa kwenda bungeni kwa maofisa kuchangiwa? Malipo yote ni sehemu ya matumizi ya wizara na kwa hivyo wizara hulipia au wahusika hulipa wenyewe na baadae kudai pesa zao wizarani wanaporudi katika kazi waliyokwenda kufanya. Sasa ni gharama gani ambazo taasisi zinatakiwa kuchangia?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 20, 2011

    Nakubaliana na mistari miwili ya mwanzo ya mchangiaji wa mwanzo katika mada hii.

    Kwa mujibu wa barua iliyowekwa hapa ni wazi kabisa kuwa huu mtindo ni wa kawaida na sio mara ya mwanzo. Neno "kama kawaida" ndio linaashiria zaidi kuwa huu ni mchezo wa kila mwaka.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 20, 2011

    Huyo Mbunge aliyetaka kuhongwa ajitokeze, huu ni utoto tu, wanaacha kujadili masuala ya msingi ya ukosefu wa umeme na kuanza kujadili chuki binafsi. Hakuna yoyote hapa, tusubiri tuone.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 20, 2011

    Hacha kusema uongo wewe. Perdiem haindi hivo. Kila idara inagharimia watu wake hizo pesa ni za kuhonga wabunge period. Per diem gani billion moja. Yani unataka kunambia TANESCO wakienda dodoma wanalipwa na wizara au TANESCO? Hacha kuleta utetezi wa kitoto

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 20, 2011

    Watanzania huu ni mchezo wa kuigiza,Sasa hawa Takukuru watasema nini? Mambo yako wazi ila mwisho wa siku Takukuru watasema hakuna kitu chochote sasa mimi sioni kabisa kama Takukuru watasema ukweli bali wao watatetea na kusema hakuna rushwa sasa Watanzania wenzangu huu ni mchezo wa kuigiza tu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 20, 2011

    Hapa Mhe. Shellukindo amekurupukia issue ambayo hajaifanyia utafiti wa kutosha. Hii inaweza kumrudia, tusubiri tuone.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 20, 2011

    tunaomba jamani wizara hiyo isafishwe kuanzia ngeleja na watu wake wote,yaani makatibu na wakurugenzi na mtunza hazina mkuu wanajua nini kinaendelea katika wizara hiyo

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 20, 2011

    Barua nimeisoma,ni kuwa kama nilivoelewa ni kila wizara ina utaratibu huo,na sio nishati tu.hivyo isiwe issue bure,ni kitu kinafanywa na wizara zote,kuwa taasisi zilizo chini ya wizara zichange pesa za wanaoambatana na waziri.sio nishati tu,hivo nishati isiwe ndo kafara wa hili jambo.nishat imekuwa mbaya zaid kwa kuwa kuna tatizo la umeme na wala si vinginevyo.embu chunguzeni wizara zote kama zinafanya hivo ijulikane serikali ndo utaratibu wake.wananchi tuelimishwe hilo,kuwa bajeti inatoka kwa pesa,au ndo watu wanavuna kama ilivyo ada kuwa msimu wa bajeti ni wa kuvuna!!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 20, 2011

    Hiki ni kimemo chenye bahasha nzuri ndan yake ni ufisadi wa hatari.
    1.Mfumo wa perdiem hautolewi hivo.
    2. Kiasi cha fedha kinatilia shaka dhidi ya matumizi yake.
    3. Mzee pinda namheshim cna, ni msomi na inteligensia mzur cna, hajakurupuka aliposema angekuwa yeye basi jairo angejikuta anapga story na familia the whole day.
    4.Kuna uwezekano hata shellukindo alihofia tu kutaja, ila anajua matumz yake.(ALIGUNA KUYATAJA KAMA ULIMSIKILIZA KWA UMAKINI).
    5.Uwekaji wa fedha ile ni kwa machale, pia taarifa irudi DP Then what next?
    Rai yangu kwa watanzania wote, usijadili jambo kama mtu aliyekatwa kichwa, fanya risearch then put comment. Angalia wabunge Wa CHAMA CHA MAGAMBA(CCM) Ataanza kusifia serikal utafkr yeye ni cabinet then anaponda half mbaya zaid hana suluhisho mwisho anakwambia kidumu cha magamba? let them go to hell.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 20, 2011

    Kwa mpango huu, maendeleo ya Taifa letu yataishia midomoni tu! Utekelezaji "buyu"

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 20, 2011

    Hakuna TAKUKURU wala nini. Yote ni gelesha tu.Vyombo vilivyowekwa kuyakabili hayo havi-function. Sioni maana ya kumsubiri rais wakati kila kitu kipo open. Tangu suala hili lijitokeze bungeni hao TAKUKURU wangekuwa washalifanyia kazi na Police washakamata waliohusika/wanaohusika na ukweli ni kuwa Wizara hiyo 'is just a drop in the ocean' kwani uchunguzi wa kina ukifanywa kikamilifu na idara zinazohusika I can g'tee you kuwa kuna Wizara nyingi zenye mchezo huo.Waziri Ngeleja kweli hatambui suala hilo? Management? Nani kawajibika mpaka sasa? Nimesoma ktk blog hii kuwa Meya wa Ilala anakwenda kusomea/workshop US kuh Accountability; Labda wangeanza kwenda Viongozi wetu kwanza. Bunge limevunja trust na wananchi wake kuh bajeti zote na ingekuwa vyema uchunguzi ufanyike kwanza kwa kila bajeti iliyopitishwa. It is high time waananchi nao waandamane (kwa kibali/ruhusa) kupinga kuendelea kwa mambo haya ya kitoto.Kwani ni sisi ndio tunaoumia kama bajeti haija-reflect the real thing.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 20, 2011

    Mh Shellukindo atuambie jee kila Idara ni kweli imetoa hizo shilingi milioni 50? Na jumla ni ngapi zilizopatikana na siyo kupiga mahesabu ya hewani tu.

    Kwa mwaka huu wa fedha hao Waheshimmiwa Wabunge wanaelewa vizuri kwamba hakuna kilichoingia huko Serikalini (OC), jee hao Maofisa wangekwenda kivipi huko Dodoma?

    Hivi kama hiyo Wizara haikupeleka maofisa halafu na wao masuali yao hayakujibiwa si ndiyo wangesema wamedharauliwa? Mimi sioni kosa la Mzee Jairo hata kidogo kwani hiyo fedha imepita kwa DP na hakuiweka kwenye akaunti yake binafsi. Na inawezekana kabisa kwamba kulikuwa na kikao na wakakubaliana kiwango na ndiyo yeye akaandika barua.

    Nyinyi wengine ndiyo musikurupuke kwani hivyo vikao vya wabunge vya kamati huwa vinaendeshwa bure bure? Wanajaribu kujizimua tu hao eti rushwa rushwa na wao wanataka walipwe posho za vikao vya kamati hata kama hawakuhudhuria. Tunayajua hayo ila huyo Mzee wa watu Jairo ndiyo amekuwa kondoo wa kafara.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 20, 2011

    TANZANIA BILA UMEME INAWEZEKANA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 20, 2011

    Wewe Anon JUl 20,05:45:00PM 2011 una pointi nzuri sana..ila ni bahati mbaya watu wengi wanaweza wasikuelewe(Jaziba)..Mimi nimekuelewa vizuri..haiwezekeni huyo Jairo atoke usingizini atume hicho "ki-memo"

    David V

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 20, 2011

    Kuna uhusiano gani na hiyo Geologic Survey of Tanzania? Mbona ameomba pesa ziwekwe huko? Ina maana ndo walaji wenzake walipo? Kweli duniani kuna mambo. Haya mkamateni na mumshughulikie haswaaaa...!! Najua mzee Peter Pinda alikuwa tayari ana deal ya kumshughulikia ila Kikwete anataka kupooza sijui? mbona amesema wasubiri? au anataka kuwakamata na wahusika wengine? Yetu macho....!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...