Semina na mitihani ya utimamu wa mwili (Physical Fitness Test) kwa waamuzi wa daraja la II na III iliyopangwa kufanyika Agosti 2 hadi 5 mwaka huu katika vituo vya Dodoma, Mwanza na Ruvuma imeahirishwa.

Hivyo waamuzi wote waliotakiwa kushiriki katika semina hiyo ambapo pia watajitegemea kwa usafiri, chakula na malazi wanatakiwa kusubiri hadi hapo itakapotangazwa tarehe nyingine.

Semina na mitihani hiyo itakwenda sambamba na shughuli ya upandishaji madaraja kwa waamuzi ambao watafaulu. Hivyo tarehe nyingine ya semina itakapopangwa, wahusika wataarifiwa mara moja.

Nayo kozi kwa ajili ya watathimini wa waamuzi (referees assessors) inayoendeshwa na wakufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itafanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 30 hadi 31 mwaka huu.

Watathimini 20 wa waamuzi watashiriki kozi hiyo itakayofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wote ni waamuzi wastaafu.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...