WOMEN in LAW and DEVELOPMENT in AFRICA (WiLDAF)
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------SHIRIKA LA WANAWAKE KATIKA SHERIA NA MAENDELEO AFRIKA
Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF)
linawakaribisha mashirika, vikundi, taasisi na wadau mbalimbali kushiriki kongamano la Siku ya Wanawake wa Afrika. Kongamano hilo litafanyika katika Viwanja vya Karimjee tarehe 2 Agosti, 2011 kuanzia saa 03:30 asubuhi. Aidha wadau wote wenye nia ya kutoa huduma mbalimbali au kuonyesha kazi za mashirika/vikundi vyao wanakaribishwa kusajili majina yao katika ofisi za WiLDAF, zilizoko Mikocheni “A”, kabla ya Jumatatu tarehe 1 Agosti, 2011.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...