Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) kinapenda kuungana na watanzania wote kulaani kitendo cha Kinyama alichofanyiwa Mpigapicha wa Gazeti la Majira na Mwandishi wa Sani, kwa kuvamiwa na wananchi, kupigwa na kuporwa mali zao wakati wakiwa kazini kuripoti tukio la vurugu za kundi la vijana waliokuwa wakishambulia polisi kwa mawe baada ya Polisi kuchukua Mwili wa Marehemu Bakari Hamisi ambaye ndugu zake waligoma kuu zika Julai 6, 2011.

Kitendo walicho fanyiwa Wanahabari hao ni cha Kinyama na katu hakiwezi kuvu milika.
Hivyo tunaliomba Jeshi la Polisi lifanye kazi yake ipasavyo na kuhakikisha wote waliofanya vurugu hizo wanapatikana na kufunguliwa mashitaka kwa vitendo hivyo vya vurugu na kujeruhi watu na kuharibu mali.

Kumekuwapo na vitendo vingi vya kinyama wanavyofanyiwa Waandishi wa Habarui hasa Wapigapicha kwa kupigwa na wananchi ama Polisi ambao kimsingi wanajua kazi na wajibu wa Wanahabari katika jamii.

Pia hivi karibuni, katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Mpigapicha wa Mwananchi Communication Fidelis Felix akiwa kazini alishambuliwa na kuharibiwa Camera yake na Askari.

PPAT inapenda kuliomba Jeshi la Polisi kutoa elimu kwa Askari wake kuwa Mwandishi wa Habari si mtu wa kubugudhiwa na kupigwa wakati wanafanya kazi zao kwani kufanya hivyo ni kuinyima haki jamii kupata habari mbalimbali zinazo tokea katika jamii.

PPAT inawapa pole Heri Shabani na Christopher Lissa kwa mswaibu yaliyowafika na Mungu awape nguvu na kurejea tena katika kazi.

Mroki Mroki
Katibu Mtendaji PPAT.
0717002303/0755 373999

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Askari aliyempiga mwandishi wa habari si yupo na anajulikana kwa nini nyie PPAT MSIMSHITAKI huyo askari kwa kutumia mwanasheria.
    Ifike wakati sasa mfanye kazi kisayansi sio kiuswahili uswahili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...