Na Woinde Shizza,Arusha
Timu ya TSC Sports Accademy ya mkoani Mwanza imeendelea kufanya vyema katika mashindano yake ya Rolling stone yanayoendelea jijini hapa mara baada ya kuinyuka timu ya kutoka nchini Burundi bao 1-0 mechi iliyochezwa katika kiwanja cha kumbukumbu za Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Katika mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kusisimu timu ya TSC Spots Accademy iliweza kuanza vyema mchezo huu na ilipotimu dakika ya 23 ya mchezo timu hii iliweza kujiandikia bao la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Tito Jonathan ambaye aliunganisha pasi moja ambayo ilimshinda golikipa wa timu ya Burundi kuokoa.
Hadi kipindi cha kwanza kumalizika timu ya Burundi iliambulia patupu na timu ya TSC ilikuwa ikiongoza kwa bao moja,walipo rudi kipindi cha pili timu zote zilikuwa zimejipanga vyema hali iliyosababisha hadi dakika 45 za kipindi cha pili kumalizaka timu zote kutoka bilabila.
Ripota wa Globu ya Jamii aliongea na kocha wa timu ya TSC sports Accademy, Jocky Dominic naye alisema kuwa mashindano haya ni mazuri na wanategemea kucheza vyema ili kutengeneza ushindi na kombe la mashindano haya na kulipeleka mkoani Mwanza.
Alisema kuwa mashindano haya ni mazuri kwani yanawapa vijana wao fursa ya kukutana na vijana wengine ambao ni wachezaji na kubadilishana nao uzoefu na ujuzi katika swala zima la mpira.
Alibainisha kuwa pia mashindano haya ni mazuri kwani yanawasaidia vijana hao kupata soko la kimichezo na kuweza kuchukuliwa na na timu kubwa ambapo baadae wataenda kucheze huko na watakuwa wamejikwamua kimaisha na wamepata njia ya kujitengenezea maisha yao ya baadae.
Alitoa wito kwa wadau wa soka wa mkoa wa Arusha na wa nje ya mkoa huu kujitokeza kwa wingi kuangalia vipaji vya vijana hapwa ambao ndo kwanza wamechupukia katika michezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...