Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Precision Air, Bw. Alfonse Kioko, ndani ya Power Breakfast Show. Kulia ni Mtangazaji Gerald Hando na katikati ni Paul James maarufu kama PJ kutoka Clouds FM.
Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Precision Air, Bw. Alfonse Kioko akihojiwa na Babbie Kabae katika kipindi cha asubuhi cha Choice FM.
Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga (Kulia) na Bw. Ruge Mutahaba (Wa pili kulia) katika mazungumzo na ujumbe kutoka Precision Air.
Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga. Bw. Kioko pia alimshukuru kwa ukarimu na ushirikiano mzuri Clouds Entertainment waliohuonyesha kwa Precision Air toka waanze kushirikiana pamoja.
Kutoka kushoto, Meneja Masoko wa Precision Air Bw. Emillian Rwejuna, Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko, Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Bw. Phil Mwakitawa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko na ujumbe wake wakiagana na Bw. Joseph Kusaga nje ya ofisi za Clouds Media Group eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Picha na John Bukuku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...