Balozi Mwanaidi Maajar-Sinare  akizungmza na wana habari baada ya chakula cha pamoja kati ya wakuu hao wa makampuni pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara na maafisa wa bodi ya utalii nchini.
Mwenyekiti wa C.T.I Bw Anup Modha (kulia) na Afisa Ubalozi wetu Marekani Suleiman Saleh   (shoto)wakiwa na mwenyekiti wa kampuni ya kufua umeme ya Symbion Power Bw Joseph Wilson

Mwenyekiti wa C.T.I Bw Anup Modha akibadilishana kadi na balozi wa Tanzania nchini Marekani  Mh.  Mwanaidi Maajar- Sinare  wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa wakuu hao.
Wageni walipata fulsa ya kubadilishana mawazo .
Mwenyekiti wa C.T.I Bw Anup Modha akiteta jambo na mwenyekiti wa kampuni ya kufua umeme ya Symbion Power Bw Joseph Wilson
Bw Erick Pike (Mwenye koti la rangi nyeusi)akitoka katika hoteli ya East Africa akiwa ametanguliwa na mwanae mara baada ya chakula cha pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara na maafisa wa bodi ya utalii.
Wageni wakibadilishana mawazo.
Balozi Majaar katika picha ya pamoja na wageni waliohudhulia chakula cha mchana kati ya wakuu hao wa makampuni pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara na maafisa wa bodi ya utalii.

Habari na Picha na Dixon Busagaga
Globu ya Jamii, Arusha
---
BALOZI wa Tanzania nchini Marekani Bi Mwanaidi Maajar pamoja na ugeni wake leo wamekula chakula cha pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara pamoja na maafisa wa bodi ya utalii Tanzania katika Hoteli ya East Africa.

Ugeni huo ambao ni Marais,wenyeviti na wakurugenzi wa makampuni mbalimbali ya nchini Marekani wako nchini kwa ziara maalumu iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuja nchini kuangalia maeneo kwa ajili ya kuwekeza pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza baada ya chakula ,Rais wa kampuni ya usafirishaji ya Ahmed’s Moving Express Inc,Bw Ahmed Issa , mtanzania aliyehamia Marekani kwa zaidi ya miaka 20 amesema Tanzania ni moja ya nchi yenye rasilimanli nyingi pamoja na mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji.

“Mimi ni mwenyeji wa Tanga naamini nina wajibu wa kurudi nyumbani na kuwekeza na hatua hiyo imekuja baada ya kuonana na balozi wa Tanzania nchini marekani ,lakini pia niliwahi kuonana na viongozi wa juu wa serikali ambao nilishauriana nao na kukubali mwaliko wa kuja nchini kujionea hali halisi ya mazingira ya uwekezaji”alisema Issa.

Kwa upande wake Erick Pike ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya umeme ya Pike amesema kampuni yake inatarajia kuwekeza katika miradi ya umeme na kuboresha miundombinu iliyopo hasa katika mikoa ya kanda ya kati.

“Tumeelezwa kuhusu tatizo la umeme nchini Tanzania.tunatarajia kushirikiana na Tanesco katika kuboresha miundo mbinu na kuzalisha umeme”alisema Pike.

Naye mtendaji wa mtandao wa Hotel za Camden Bw Munir Walji amesema kampuni yake imepata maelezo ya kina kuhusu maeneo ya uwekezaji na kwamba ikipata ardhi itajenga hoteli mbili zenye hadhi ya nyota 5
katika jiji la Dar es slaam na Arusha.

Munir amesema ili kuunganisha hoteli hizo na sekta ya utalii,kampuni yake inatarajia kujenga hoteli nyingine ndogo katika maeneo ya jirani na hifadhi za taifa na mbuga za wanyama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...