Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) na Naibu Waziri wa Utamaduni China Mhe. Madam Zhao Shaohua wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa maonyesho ya picha za kuchora ambazo ni matunda ya mradi wa African Arts-in-Residence ulioratibiwa na kufadhiliwa na Wizara ya Utamaduni China. Uzinduzi huo ulifanyika jana jioni Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Utamaduni wa China Mhe. Madam Zhao Shaohua (mama aliyenyosha mikono) na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) (aliyevaa tai nyekundu) wakipewa maelezo kuhusu picha za kuchora ambazo ni matunda ya mradi wa ‘African Arts-in-Residence’ ulioratibiwa na kufadhiliwa na Wizara ya Utamaduni China, mara baada ya uzinduzi wa Maonyesho ya picha hizo yaliyofanyika Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam jana jioni. Mradi huo uliwashirikisha Wasanii 15 kutoka nchi 15 za Ki-Afrika, Tanzania ikiwa moja wapo, Mradi huo ulilenga kuelezea kwa njia ya picha za kuchora jinsi Wasanii wa Afrika wanavyoiona nchi ya China.
Naibu Waziri wa Utamaduni wa China Mhe. Madam Zhao Shaohua (mama aliyevaa sketi nyeusi katikati) na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Picha za Kuchora ambazo ni matokeo ya mradi wa ‘African Arts-in-Residence’ ulioratibiwa na kufadhiliwa na Wizara ya Utamaduni China ambapo Wasanii 15 kutoka nchi 15 za Afrika walishiriki katika mradi huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...