Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Kivukoni na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salimu akizindua maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho leo jijini Dar es salaam. Chuo hicho kimeanzishwa tarehe 29 Julai mwaka 1961.Wageni wengine ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba .
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akitoa mada juu ya mchango wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika maendeleo ya Taifa leo jijini Dar es salaam wakati wa uzindua maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho . Chuo hicho kianzishwa tarehe 29 Julai mwaka 1961.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Kivukoni Dkt John Magotti akitoa hotuba ya ukaribisho leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uanzishwaji wa Chuo hicho.
Mawaziri Wakuu Wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) na Dkt Salim Ahmed Salimu(kulia) wakibadilishana mawazo leo jijini Dar e salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uanzishwaji wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kivukoni.
Wanajumuiya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Kivukoni wakicheza muziki leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho .
Wanajumuiya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Kivukoni wakimsikiliza kwa makini hotuba ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim(hayupo pichani).Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2011

    Safi sana.Kwa hali ilivyo kwa sasa tunahitaji rais 2015 atoke kwenye kundi la watu wenye mawazo ya "Kinyererenyerere".Liwalo na liwe

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2011

    Safi sana !Miaka 50 ya chuo ,miaka 50 ya Uhuru,lakini nini tumejifunza ?
    Waliohitimu wamefanya nini au wanafanya nini katika maendeleo ya nchi?
    Tutabakia kusherehekea kitu kisichokuwa na manufaa yoyote,maji umeme,madawati,madawa hakuna.
    Labda tumejifunza kugawana mali za serikali kama majumba na viwanja na kupiga deal za kuuza malia asili na madini.
    Siasa imezidi sana kuliko mahitaji muhimu ya wananchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...