Meneja wa Vodashop Mlimani city,Fatma Kalyanye akiwaelekeza warembo wa Vodacom Miss higher learning waliozuru duka hilo namna ya kuweka nyaraka za kudumu za wateja wao wa M-pesa, warembo hao walitembelea makao makuu ya kampuni hiyo ikiwa ni moja ya hatua za kuelekea kilele cha shindano lao liatakalofanyika mwishoni mwa wiki mjini dodoma.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja Bw. Hiramu Mungai akitoa ufafanuzi wa jinsi ya kutoa huduma kwa wateja kwa Warembo wa Vodacom Miss higherlearning waliokuwa katika ziara ya kutembelea makao makuu ya kampuni hiyo.
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania Najenjwa Mbaga akisalimiana na warembo wa Vodacom miss higherlearning walipozuru makao makuu ya kampuni hiyo wakiwa safarini kuelekea mjini Dodoma katika fainali za shindano lao litakalofanyika mwishoni mwa wiki.
Mfanyakazi wa Vodashop Mlimani City Jane Mrosso Akiwapa maelekezo ya matumizi ya simu mbalimbali baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Higher learning walipotembelea duka hilo, ikiwa ni hatua mojawapo ya kuelekea katika shindano lao linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Higher learning waliokuwa katika ziara ya kutembelea Makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo shindano lao linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Higher learning wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2011

    Wote wazuri, hohoho!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2011

    haya, kikao chema cha bunge.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2011

    ankal sikamooo.picha ya tano kutoka juu mrembo wa pili toka kushoto anaweza peperusha bendera yetu ya taifa mbali.mdau ughaibuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...