·         Ni kupitia Tangazo la luninga la Airtel linafanya vijana kuwa na shauku kubwa ya mpira wa miguu na matokeo ya  kupitia Airtel Rising Stars.
·         Tangazo la Airtel kwenye luninga ni kiashirio kizuri jinsi Airtel ilivyojikita na kuendeleza vijana wenye vipaji katika nchi 15 ambazo Airtel inafanya biashara.
·         Michuano ya Airtel Rising Stars ni mpango unaosaidiwa kwa pamoja na Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester United ya Uingereza

Airtel Tanzania, Agosti 16, 2011 – Hivi karibuni Airtel Africa imezindua tangazo la luninga kwa Afrika nzima ambayo madhumuni yake ni kuhamasisha vijana kuwa na shauku ya mchezo wa mpira wa miguu kwa kushiriki kwenye michuano ya Airtel Rising Stars. Michuano hiyo, ambayo kwa sasa inaendelea kwenye nchi 15 za Afrika ambapo Airtel inafanya biashara, ina lengo la kutafuta na kukuza vipaji vya mpira wa miguu kuanzia ngazi ya chini.
 ‘Airtel ina shauku kubwa sana na Afrika, na Afrika ina shauku kubwa sana na mpira wa miguu’. Mpango kama huu unaifanya jamii inayotuzunguka kuwa na mtazamo chanya na kuwawezesha vijana kujiendeleza kupitia mpango huu wa Airtel Rising Stars, anaelezea Andre Beyers, Meneja Masoko wa Airtel Afrika.

Akielezea juu ya hilo tangazo la luninga, Bw. Beyers alisema: Kinachofanya michuano ya Airtel Rising Stars kuwa tofauti na michuano mingine ya mpira wa miguu ni jinsi mpangilio mzima na upana wa mpango huu. Michuano hii inachezwa na maelfu ya vijana Bara nzima la Afrika na inatia moyo sana. Huu ndio ujumbe tunaotaka kuufikisha kwa kupitia tangazo hilo.

Tangazo hilo linaanzia kwa watu binafsi katika mandhari mbalimbali katika bara huku wakitazama ndege ikuruka juu. Ndege hii inaangusha maelfu na maelfu ya mipira kwenye Kata tofautivijijini na mjini, kwenye milima na mabonde na pia kwenye jangwa. Wakati wa kudodosha mipira, mpira mmoja unajitenga kutoka kwenye mipira mingine na kuanza kusonga mbele peke yake kupitia kwenye mitaa na vichochoro. Hatimaye unasimamia kwenye miguu ya mwanafunzi akiwa kwenye kiti chake cha kusomea.
Tangazo linaishia kwa ujumbe usemao, ‘Kama wewe ndio staa wa Afrika unayefuata, basi tutakufikia.’ Michuano hii tayari inaendelea kwenye nchi 15 barani Afrika, ambapo timu zaidi ya 3,000 zinashiriki.

 ‘Michuano ya Airtel Rising Stars imejikita kwenye kutafuta na kukuza vipaji vya soka kwa vijana wenye umri chini ya 17 ambapo pia watapata nafasi ya kuonyesha umahiri wao kwa wataalamu na waalimu wa mpira wa miguu’ anasema Cheikh Sarr, Meneja Masoko wa Airtel Tanzania na kuongeza kuwa kwa hapa Tanzania peke yake, timu 24 zilishiriki kwenye ngazi ya mkoa ambapo timu 4 bora zitasonga mbele kwenye ngazi ya Taifa. Tunatarajia kufanya  kazi kwa ukaribu na wachezaji wanaoshiriki kwenye  michuano hii na kuwapa nafasi ya kukuza vipaji vyao.

Kwa hapa Tanzania, Airtel Rising Stars ni mpango wa Airtel pamoja na Klabu ya Manchester United. Ushirikiano huu na Manchester United ni mpango wa miaka minne uliosainiwa Desemba mwaka jana.  Manchester United kwa kutumia nembo yake ya shule za soka ya aegis itatoa msaada wa kiufundi katika kambi za soka zitakazofanyika Gabon na Tanzania mwishoni mwa mashindano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...