Assalam aleikum ankal

Naomba msaada kwa wadau wote, ila jina langu weka kapuni maana hata mwajiri wangu wa sasa hajui kama nimepata kazi sehemu nyingine ntamfahamisha mambo yakiwa sawa Inshaallah, nimepata bahati ya kuitwa kwa induction course kwenye moja ya nchi za umoja wa schengen. Msaada ninaouomba ni huu, nimekataliwa visa na sababu niliyopewa ni kwamba sikuwa na pesa ya kutoka kwenye account yangu, na pia hawakuridhika kamakweli nitarudi, lakini ajabu ni kwamba mwajiri wangu mpya  alinitumia vifuatavyo,

1)       Invitation letter ( wakijicommit kwa gharama zote za usafiri, insurance, malazi, chakula)
2)       Travel isurance ya euro 1m
3)       Return ticket ( KLM)
4)       Hotel booking
5)       Travel information
6)       Two weeks course plan

Nikaandika barua, nikalipa ada ya kuomba na kila kila kitu

AT THE END WAKA REFUSE, Na kunifahamisha kama sijaridhika na waweza ku appleal au kuomba reconsideration, nimeomba reconsideration ila dalili naona kama sio nzuri maaana kila nikipiga kuulizia naambia hatujapata muda wa kuyapiatia maombi yako

Nifanyeje wadau?? Nami nilikua naenda huko ili baadae niwe deployed Somalia


Mzee wa Bunju

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Naomba sana sana ndugu uhakiki kwanza habari za huyo mwajiri wako mpya, utapeli ni wa kutosha sana siku hizi, wengine wakitumia majina ya UN kutapeli watu, jitahidi sana kufuatilia ukweli wa hayo mambo na ikiwezekana utumie hata ubalozi wa hiyo nchi unayotaka kwenda kama upo hapa nchini kwetu upate uhakika kabla hata hujaanza kuhangaika na visa. Ni ushauri tu.

    ReplyDelete
  2. Hiyo invitation letter haitoshi mzee. Kinachotakiwa wakupe barua tofauti inayoonesha kuwa umepata scholarship. (Mdau Stockhom hapa)

    ReplyDelete
  3. Wewe umekataliwa kwa sababu ni kweli hutarudi si unaenda kufanya kazi??? Pili hiyo insurance ya 1m euro nao ni utata mtupu; ni kubwa saaana na labda imewafanya wa daubt information nyingine zoote. Pili its true kuwa hawa jamaa ni wepesi sana kutoa au kukunyima visa mfano mimi nina rafiki zangu wanakujaga sana kunitembelea huku Holand; but wanapewa visa kwa kuwa wako settled back home. Sasa kama hata kipato chako hakieleweki lazima wakushuku. Vile vile siku hizi wahamiaji haramu wanapingwa sana nchi za Ulaya; hence pole ndugu.

    ReplyDelete
  4. Mdau pole sana. Mimi nafanyakazi hapo ubalozini na nimeshakushitukia. Sasa kijana nikiangalia hayo maombi na kila kitu kimetimia. Lakini jiulize wewe hapo umewekewa "insurance" ya 1M Euro kwa course ya wiki 2, pili kama ni kijana pia watakuwa na wasiwasi, tatu wanaokukatalia ni wabongo wenzako ndio maana ukiuliza wanakuletea longolongo. Kwa ufupi kwa uzoefu wangu na maombi ya visa kama kila kilichotakiwa umekamilisha basi hakuna sababu ya kukukatalia kwani sikuhizi wanachotaka ni ukamilishe masharti, hao watakuwa wabongo wenyekufanya kazi hapo ubalozini. Kwani sasa Europe wana software ambayo inachukua madole yako tena ukiingia nchi moja zote tayari wanayapata. Sasa ushauri wangu kwa njia niliyotumia mimi andika email moja kwa moja kwenye ubalozi ya kuuliza kuwa umeomba "reconsideration" je majibu vipi. Usijaribu kuongea na wabongo maana ndio wanaoharibia watu. Kitu muhimu kila wanachotaka ukikamilishe. Angalia vizuri pengine hukukamilisha vitu vinavyohitajiwa, pia mwajiri wako muulize pengine nae alipoulizwa kuhusu wewe kasema kitu kibaya.

    ReplyDelete
  5. hizo document zako zinatosha kwa visa. wewe umetapeliwa kwa ajira "hewa", ukiwapigia simu hao waliokualika utakuta wako west africa

    ReplyDelete
  6. Anonnymous wa 11:22:00pm sehemu ya maoni yako siyo sahihi. Pamoja na kufanya kazi ubalozini (igawa hukuandika upo ubalozi gani na kitengo kipi) nafikiri huelewi kuwa sheria inaruhusu mwombaji yeyote kukataliwa viza hata kama amekamilisha masharti yote yanayotakiwa na hana kosa lolote. Visa is not an applicant's right, it is only a privilage.Kwahiyo naomba nitofautiane wewe(ofisa ubalozi) kuwa anaposema "..kama kilichotakiwa umekamilisha basi hakuna sababu ya kukukatalia..." Hayo maelezo siyo kweli. kama huamini,kaulize cansulate section hapo kazini kwako.Although I don't know the flip side of the applicant's story,to my opinion,most of visa applicants rely on documents and forget that those documents cannot speak for themselves.In most cases, cansulars like to see a confident applicant who express him/herself while maintaining an eye contact during an interview. Critical thinking and logical reasoning can also help (this reffers to the US embassy where I obtained my US visa).Lastly, I did not understand whem mdau said waliokunyima viza ni wabongo...na maoni yao kuyaita longolongo.Kwani wewe unatoka nchi gani? Pamoja na maelezo yako yasiyo sahihi, hakuna aliyekuita muongo. Unaweza kutofautiana na maoni ya wadau, lakini sidhani kama ni sahihi kusingizia "wabongo" eti wamenyima viza muombaji. Mdau DC

    ReplyDelete
  7. Ingekuwa bora ungetaja jina la nchi ambayo umeomba viza na kujimwa. Ita kuwa rahisi ukiwa muwazi zaidi.

    ReplyDelete
  8. Hawa watu ni wabaya jamani. Ukitaka visa ya kwenda bongo wiki ushapewa. Sisi tukitaka kuja kwao unanyimwa visa, wanatuzarau na kutudhalilisha wakati mwingine. Nchi yetu na iamke jamani.

    ReplyDelete
  9. OMBA HIYO KAMPUNI WAKUTUMIE COMPANY CERTIFICATES, then zipeleke kuattach kwenye yale maombi yako,na kumbuka kama wanahisi unaenda kufanya kazi hawawezi kukupa bila hiyo kampuni wanayokuita kuwatumia STR copy, hiyo wanatuma direct to the embassy then wewe wanakutumia copy,STR ni subject to regularization.pia na your credentila certificates na CV, inawezekana kwa upande wako hukujikamilisha.kuwa mkweli, kama unaenda kufanya kazi na hutarudi tukupe requrements sahihi.kwa hiyo insurance inasema kabisa kuwa you are going for a long time, not just two weeks.

    ReplyDelete
  10. MZEE WA BUNJUAugust 23, 2011

    NIMERUDI TENA, UNAJUA NAONGOPA TU KUDISCLOSE MAANA NAJUA WASOMAJI WA BLOG HII WENGINE NI WAFANYAKAZI WA EMBASSY HII HUSIKA,HUYU MWAJIRI WANGU NILISHAFANYA NAE KAZI KWA MIAKA 9 KUANZIA KASULU KIGOMA, MTWARA NA DAR ES SALAAM NIKIWA KAMA CAPITAL LOGISTICIAN, WANANIFAHAMU VIZURI, INTERVIEW NIMEFANYA KWA SIMU, ONLINE, NA NIMEENDA NAIROBI KWA INTERVIEW YA SIKU MBILI, MAANA ILIKUA NI WRITTEN NA ANA KWA ANA, NIKAFAULU, NA SI MARA YA KWANZA KUWA INVITED NA HUYU MWAJILI, NILISHAKWENDA COURSE NYINGINE BELGIUM KABLA SIJAPANDISHWA CHEO, ILIKUA MWAKA 2004. KWA SASA HAWA JAMAA WALIFUNGA OFFICE HAPA TANZANIA , NA NINAFANYA KAZI NA SHIRIKA JINGINE, NA WANATAKA KUNIAJIRI KAMA INTERNATIONAL EMERGENCY STAFF WAO, KILA KITU KIO READY TABU NI HII VISA. IMMA KUHUSU INSURANCE YA 1M SIO ISSUE MAANA NI STANDARD YAO NA MIMI NAJUA MAANA NILISHAFANYA NAO HAWA, NA KWA KWELI SHIRIKA HILI NI KUBWA SANA DUNIANI LAKINI SI UN, NA LIKO NCHI ZAIDI YA 60, NA OPERATION SECTION ZIKO 5 IKIWA NI PAMOJA NA SPAIN, FRANCE, BELGIUM, GREECE,HOLLAND,, SASA MIMI NIMEPTA NCHI MOJA KATI YA HIZO

    NISAIDIENI,

    ReplyDelete
  11. Travel insurence ya EURO 1M? Maswali yote yanaanzia hapo! Pia acha kuficha habari. Nchi gani? Course gani? Mwajiri hawezi kujua kwa wewe kuandika taarifa kama hizo, Woga na siri zisizo na mapango ndiyo silaha za matapeli!

    ReplyDelete
  12. Kuna jambo ambalo linasababisha hadi hii neema uliyotaka kupewa na Mungu ionekane vigumu kwako ndugu yangu.Sijui unaabudu dhehebu gani,ila nadhani unatakiwa uwe mkweli linapokuja suala la ukweli.Simaanishi uwe muongo linapokuja suala la uongo la asha!! kuwa mkweli hadi kufa.
    Ushauri,1]kuwa mkweli na muwazi kwa mwajiri wako!!
    2]Induction course inatanguliwa na barua ya ajira husika,barua ya ajira ndiyo inekusaidia kupata visa.Halafu cha kushangaza ni two weeks course plan kama nyaraka waliyo kutumia wakati umepata ajira[inashangaza] nadhani hata afisa wa ubalozi aliyesoma Gumbaru hakubaliani na hilo.
    3]Unaiambia jamii kuwa baada ya kufika huko,nia yako ni kuwa deployed Somalia,hapa pia umedanganya[Somalia na Schengen countries wapi na wapi?.Unless basi inaonekana hauridhiki na ajira zako na sehemu unayopangiwa na mwajiri wako.Ni mapema kutwambia hilo mtandaoni.Ndo maana bado nasema mambo yako yanakuwa magumu.
    4]Kwa kina nadhani pande zote mbili ie:wewe na anayedhaniwa kuwa mwajiri wako mpya kuna udanganyifu.
    Mwisho,Sikukatishi tamaa ila suala la kusafiri nje ya nchi yeyote linahitaji taarifa sahihi na zenye kushabihiana kwa kila nyaraka.
    Ubarikiwe!!na fikiria zaidi. thinkers_global@yahoo.com

    ReplyDelete
  13. Mimi kwa experience yangu yaani ubalozi wa Belgium ni Nooooomaa kishenzi hata uende na documents zote bado hawatakupa watakuzungushazungusha tu. Kuna mama mhindi pale utadhani analipwa kwa ajili za kuwazungusha watu. Mpuuzi sana aise

    ReplyDelete
  14. Kwa sisi wataalam wa bima kuwa na bima kubwa ya euro 1m ni kubwa mno ni kama bilioni tatu za tanzania ina maana bima kubwa hatari kubwa.Bima kubwa hivyo ina maana wewe ni mtu wa risk kubwa.Nadhani ndio maana wamekukatalia.Risk yako ikitafsiriwa kipesa za bima inatisha.Hata mimi nisingekupa visa.

    ReplyDelete
  15. Kuandika barua peke yake na kujicommit haitoshi, sponser anatakiwa athibitishe ana uwezo huo maana siku hizi kuna kampuni na vyuo feki.

    ReplyDelete
  16. My experience! Schengen countries sio wasumbufu kutoa visa nikilinganisha na USA na UK. Wao wanacheza zaidi na VISA application documents, wanaenda mbele zaidi ya invitation letter. Wakishtuka kama documents zako ni ngumu (zina ukakasi) wanakuweka kapuni. Mfano iyo Travel Insurance ya Euro 1 Million for two weeks course?, mbona ni utata? Turushie hapa kwa michuzi jina na address ya iyo kampuni iliyokuita, pamoja na copy ya iyo "Travel insurance ya 1mill Euro".Ili tuimulike iyo kampuni kwanza, mengine yatafuatia. Pia naungana na wadau waliotangulia-kuwa wazi ni nchi gani unategemea kwenda ili upata msaada wa uwakika.
    Mdau Germany.

    ReplyDelete
  17. Vipi walikuuzia tiketi wakati huna viza?

    ReplyDelete
  18. Mzee wa Bunju, kwani wewe ni dini gani? Kama ni muislam huu ni mwezi bora kuliko yote amka usiku ukikisha kumuomba Mungu akufanyie wepesi mambo yako.

    Nasema hivyo kwa sababu mimi yalishawahi kunikuta, nilikuwa natakiwa kusafiri kwenda nchi mojawapo Afrika lakini kwa usafiri wakati huo connection ilikuwa through one of the Schengen countries. Na safari zangu zote za Ulaya nilikwa sijawahi kukumbana na kituko kama nilichokumbana nacho wakati huo. Nikatakiwa nikate Schengen transit visa, basi wacha wanizungushe, nilipoona ninaweza hata kukosa kwenda kwenye huo mkutano nikaenda kwenye ubalozi wao nikawaambia nawithdrawal my visa application, nilipopata passport yangu nikaenda shirika lingine la ndege nikakata tiketi ya ndege lakini kupitia huko huko Europe ndio nikasafiri. Kitu nilichogundua kuwa nilikuwa mdomo wazi sana kuhusu safari yangu that time kuliko wakati mwingine. Watu wengine wana hasada tu ndani ya nafsi zao, cha msingi mlilie mungu wako akufanyie wepesi baada ya kupeleka vielelezo vinavyotakiwa kwani nina uhakika wakikunyima visa wanakupa sababu iliyowafanya wakunyime hiyo visa ili na wewe upate nafasi ya kupeleka hivyo vielelezo. Sasa kama umepeleka walivyokuomba na bado kuna usumbufu, omba Mungu, pia andika email kuulizia usipende kutumia simu kwani haina ushahidi wa ufuatiliaji wako na email watu huichukulia serious kuliko simu.

    Kila la kheri na mkumbuke pia kutoa zaka na sadaka sio mnafanya kazi hamumkumbi Mungu, hii yaweza kuwa your wake up call. Vile vile ikiwa utasali sala ya haja na kumuomba Mungu bado ukakwama, kaa kitako tulia uendelee na kazi yako hapo ulipo kwani Allah yuajua kipi chenye kheri kwako pengine huko uendako ni lucrative lakini hakuna salama kwako!

    ReplyDelete
  19. Travel insurance ya euro 1 m , angalia wasije wakakumaliza chunguza kwanza kunamatukio mengi sana wanaweza waka kuuwa na kupata hizo pesa binadamu siwema kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...