Afisa Mtendaji Mkuu,utawala wa kiwanda cha sukari cha TPC , JaffaricAlly akimweleza mkurugenzi wa manispaa ya Moshi,BernedetecKinabo(katikati) jinsi TPC ilivyoanza ukarabati wa barabara ya Sukari.kulia ni meneja mawasiliano na uhusiano wa kampuni ya bia Tanzania(TBL) Edithe Mushi.
Barabara ya sukari inayounganisha katikati ya mji wa Moshi na eneo la viwanda inavyoonekana baada ya kuanza kufanyika kwa ukarabati.

Picha na habari na Dixon Busagaga 
wa Globu ya Jamii, Moshi.

KIWANDA cha Sukari cha TPC Ltd wilayani Moshi,kimetoa msaada wa zaidi ya Sh Mil 16.6 kwa halmashauri ya manispaa ya Moshi kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Sukari yenye urefu wa Km 2.6 kwa kiwango cha
changarawe.

Barabara hiyo ambayo ni mhimili wa kiuchumi kwa manispaa hiyo inatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami baadaye mwaka huu baada ya kuharibika mara kwa mara licha ya kwamba ndiyo barabara pekee
inayoelelekea katika maeneo ya viwanda vya sukari, Bia,Karatasi na Mbao.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo,Bernadette Kinabo alisema  kuwa tayari manispaa imepeleka ombi kwa bodi ya barabara mkoani humo(TANROAD) na kwamba barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami kwa zaidi ya Sh
Bil 3 ikiwa ni fedha kutoka serikalini.

Alisema kutokana na umuhimu wa barabara hiyo,manispaa ilikutana na wadau kama TPC,kiwanda cha Bia Tanzania,Serengeti,kampuni za ukandarasi na asasi nyingine za kifedha ambapo waliahidi kusaidia
ujenzi huo.

“TPC waliahidi kutoa vifaa na wafanyakazi wake ambapo kwa ujumla wanachangia Mil 16.6, nasi kama manispaa tumetoa Mil 10, ujenzi utaendelea tukisubiri nguvu ya serikali”alisema Kinabo.

Alisema pamoja na wadau hao lakini pia kampuni ya ukandarasi ya Ravji imechangia vifaa huku duka la kubadili fedha za kigeni la Trust wametoa Sh mil 2.5 ambapo aliomba makampuni mengine kujitokeza
kusaidia ujenzi wa barabara hiyo.

Kinabo alisema hadi sasa manispaa hiyo imepokea zaidi ya Sh Mil 42.1 katika kuhakikisha ukarabati wa barabara hiyo unakamilika ili pia kutoa fursa za kibiashara kwa wakazi wa manispaa hiyo kwa kutumia
barabara hiyo.

Awali meya wa manispaa hiyo,Japhary Michael alisema misaada hiyo inatoa moyo kwa manispaa lakini pia inaonyesha jinsi ambavyo wadau walivyona imani na manispaa katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo kampuni ya bia Tanzania(TBL) imekabidhi hundi ya shs. Mil. 10 kwa halmashauri ya manispaa ya Moshi kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa barabra hiyo .

Meneja mawasiliano mahusiano wa kampuni hiyo, Editha Mushi alisema fedha hizo ni sehemu ya mapato ya kampuni katika kuchangia na kutatua mahitaji ya jamii kama njia moja wapo ya kudumisha uhusiano
uliojengeka kwa miaka mingi.

Alisema ujenzi wa barabara hiyo hautasaidia tu kituo cha mauzo cha TBL lakini pia wananchi wa Moshi na maeneo mengine mkoani humo watapata fursa ya kufungua biashara mbalimbali katika maeneo hayo kwa kutumia mawasiliano ya barabara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...