Na:- Azizi Simai Maelezo Pemba.
Balozi Mdogo wa China Zanzibar, CHEIN CHIN MAN amesifu uhusiano uliopo kati ya China na Zanzibar kutokana na mashirikiano makubwa waliokuwa nayo tangu Mapindzi ya mwaka 1964.
Amesema China itaendelea kusaidia Zanzibar katika nyanja mbali mbali za Maendeleo katika juhudi za kukuza Uchumi wake pamoja na Wananchi .
Balozi CHEIN ameyasema hayo katika Ghafla ya kukabidhi Hundi ya Shillingi Millioni Ishirini kwa Skuli Tatu ziliopo katika Jimbo la Mkanyageni Wilaya Mkoani Pemba kwaajili ya Vifaa vya Sayansi, Msaada ambao umetolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Kichina ya HUAWIE.
Kampuni hiyo ya HUAWIE imesaidia Fedha hizo kwa ajili ya Skuli ya CHOKOCHO,KISIWA PANZA NA MKANYAGENI baada ya kuombwa na Waziri wa Mawasiliano ya Sayansi na Teknolojia wa Tanzania.
Nae Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Muungano Tanzania Professa Makame Mbarawa Mnyaa amewataka Vijana Maskulini kuvitumia Vifaa vya Sayansi kwa kuliwezesha Taifa kuwa na Wataalamu wa fani Mbali mbali.
Waziri huyo amesema kuwa ili Taifa liwe na Wataalamu Wazuri ni muhimu Vijana Maskulini kuzitumia vyema Maabara na Vifaa vilivo kwenye Skuli zao na kuvienzi Vifaa hivyo iliviweze kuwasaidia na wengine.
Aidha Professa Mnyaa amesema Taifa lolote Duniani ili liendelee linahitaji Vijana waliofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika Masomo ya Sayansi.


Tsh. 20 million is less than $20,000. Is this from his own pocket or from the government of China?? In exchange for what??
ReplyDeleteReally do we need to publish such meager amount when what they reap from us in comparison to his/their $20,000 is just a drop in the ocean!
We need to be serious!
Homer
i agree wit you,the first coment,even they representative ,he/she might givin them concern those school $20,00o , i think this kind of joke from chinies for given them $20,000 . they have to be seriously,it's shame to publish .
ReplyDeleteLittle, little lastly make jug full.
ReplyDelete"little, little lastly make jug full" - Kide,
ReplyDeleteWell that's why people steal from us, treat us like bunch of incompetent people.Even our own politicians steal from us in broad daylight cause they know we will always find an excuse for their action