Dr Munisi Woiufoo, mratibu wa mradi wa taifa kupambana na ugonjwa wa malaria unaohusiana na unyuziaji wa dawa ya ukoko majumbani unaofadhiliwa na mfuko wa rais wa Marekani unaosimamiwa na shirika la maendeleo la marekani (USAID) akiongea na waandishi wa habaro ofisini kwake jana, mratibu huo alisema mradi huo umepunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria  mkoani Kagera toka asilimia 41.1 mpaka asilimia 5.
Baadhi ya washabiki wa soka katika manispaa ya Bukoba wakiwa wamepanda kwenye bango la matangazo liliko nje ya uwanja wa michezo wa Kaitaba wakishuhudia pambano la ligi ya mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki, tabia ya washabiki kupanda bango hilo imekuwa ikikemewa na watu wengi kwa kuwa wanaopanda bango hilo wanahatarisha maisha yao, katika mmchezo huo timu ya Bilele ilishinda timu ya Rwamishenye magoli 4-3 yaliyopatikana kwa njia ya matuta.Picha na Audax Mutiganzi,Bukoba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sana Dr. Munisi. Tunaamini unaendeleza juhudi za kuboresha masuala ya afya. Tunakumiss hapa Morogoro dokta wetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...