Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwasili katika Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo Wizara hiyo na taasisi zake 17 zipo kwa pamoja zikitoa huduma kwa Umma wakati huu wa maadhimisho ya Nane nane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bi Joyce Mapunjo (Kulia), akimtembeza Mh Rais Jakaya Kiwete kujionea kazi mbali mbali mbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya Wizara yua Viwanda na Biashara. Hapa Mh Rais akijionea mashine mbali mbali zinazotengenezwa na Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini (Camartec).
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mazao Duniani (CFC) Balozi Ali Mchumo na Mkewe wakitia saini kitabu cha wageni kabla ya kuanza kutembelea Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara katika maonesho ya Nane nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu akifurahia jambo na maafisa wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uzalishaji wa Bidhaa kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu ( Katikati) akielekeza jambo mara baada ya kupewa maelezo ya kiutendaji kutoka kwa maafisa wa Wakala wa Mizani na Vipimo wanaoiwakilisha taasisi hiyo katika maonesho ya Nanme nane.

Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara limekuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya Nane nane yanayoendelea mjini Dodoma. 

Miongoni mwa mambo yanayolipa sifa banda hilo ni pamoja na mpangailio makini wa Wizara na taasisi zake ndani ya Jengo moja, unadhifu wa hali ya juu wa mazingira ya banda hilo, ucheshi wa wataalamu wa Wizara na Taasisi zake wanaohudumia wananchi katika maonesho haya, huduma za papo kwa hapo zinazotolewa na Wizara na Taasisi zake, vikundi vya wajasiriamali wanaozalisha bidhaa za hali ya juu baada ya kuwezeshwa na Wizara na Taasisi zake kwa mafunzo na mitaji pamoja na bidhaa mbali mbali zinazozalishwa na Taasisi hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...