Wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania wa Ofisi Kuu ya benki hiyo Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wao Mkuu Dinesh Arora (mwenye miwani katikati) wakati wa hafla fupi ya kusherehekea miaka 14 ya utendaji wao iliyoadhimishwa jana katika matawi tofauti nchini.
Meneja wa tawi la makao makuu ya benki ya Exim Dar es Salaam,Eugen Massawe akikata keki huku akishuhudiwa na wafanyakazi wengine wa benki hiyo kama ishara ya kutimiza miaka 14 ya utendaji wa benki hiyo tangu kuanzishwa kwake katika hafla fupi iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya benki hiyo Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi Wetu.

BENKI ya Exim Tanzania imeadhimisha miaka 14 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo nchini. Tafrija fupi ya kusherekea tukio hilo ilifanyika katika makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Tafrija hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na wateja wake.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mkuu wa Benki ya Exim, Dinesh Arora alisema ya kwamba ni juhudi za pamoja za wafanyakazi wa benki hiyo zinazoiwezesha benki kustawi. Pia alitambua mchango wa wateja wa benki hiyo katika kukua kwa benki ambapo aliongeza kuwa wateja ni sehemu muhimu sana kwenye benki hiyo.

“Uongozi unapenda kuwashuru wafanyakazi wote wa benki ya Exim kwa moyo wao wa kujitolea na uchapakazi. Tunajivunia kuwa na wafanyakazi wanaokua kiufanisi kadri ambavyo benki inakua. Mchango wao uliojidhihirisha mpaka sasa ni wa thamani kubwa katika ukuaji wa benki na dhamana iko mikononi mwao kuikuza benki kufikia hatua inayofuata” alisema Arora.

Aliongeza kwa kusema, “Tusingekuwepo hapa bila ya ushirikiano wa wateja wetu na tungependa kutumia nafasi hii kuwashukuru wateja wetu wote kwa kuchagua kufanya huduma za kibenki na sisi”

Benki hiyo imesherekea miaka 14 huku ikidhihirisha ukuaji na uendelevu katika utendaji wake. Hivi karibuni benki hiyo ilichaguliwa katika kinyang’anyiro cha Tuzo ya Benki Endelevu ya Mwaka za Financial Times/International Finance Corporation. Tuzo hiyo hulenga kutambua benki ambazo zimeonyesha uwezo mkubwa wa kujumuisha mazingira, jamii na utawala katika utendaji wao wa biashara.

Benki ya Exim ni benki yenye umiliki binafsi iliyoanza kazi zake nchini Tanzania mnamo Agosti mwaka 1997. Benki hiyo inatoa huduma za kibenki kwa watu binafsi, makampuni madogo na ya kati pamoja na kampuni kubwa.

Benki imekuwa ikipanua wigo wake wa utoaji huduma na mpaka sasa ina matawi 21 nchini Tanzania. Benki pia ina matawi 3 njee ya nchi, matawi 2 nchini Comoro na 1 nchini Djibouti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...