WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, MOHAMMED ABOUD AKITOWA TAARIFA RASMI YA SERIKALI MBELE YA WAANDISHI WA HABARI YAKUPIGA MARUFUKU VITENDO VIOVU VINAVYOFANYWA KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI.PICHA NA HAMAD HIJA MAELEZOZANZIBAR.

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEWATAKA WANANCHI WANAOENDESHA VITENDO VIOVU HASA KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI KUACHANA NA VITENDO HIVYO MARA MOJA.

AKITOA TAMKO LA SERIKALI JUU YA VITENDO VINAVYOJITOKEZA KATIKA JAMII KINYUME NA MAADILI HASA KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI WAZIRI WA NCHI AFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS MHE MOHAMMED ABOUD MOHAMMED AMESEMA KUFANYA HIVYO NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI NA PIA AMRI ZA MWENYEZIMUNGU NA MAFUNDISHO YA MTUME MOHAMMAD (S.A.W) .

AMESEMA KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI KUMEJITIKEZA BAADHI YA VITENDO VIKIWEMO KUFUNGULIWA WA MABAA NA BAADHI YA MIKAHAWA WAKATI WA MCHANA PAMOJA NA KUONEKANA KWA WANAWAKE KUTEMBEA BARABARANI WAKIWA WAMEVAA NGUO ZISIZOKUWA NA HESHIMA.

HIVYO AMEZITAKA TAASISI ZA DINI NA ZINAZOHUSIKA NA MASUALA HAYO KUCHUKUA HATUA ZINAZOFAA KWA AJILI YA KULINDA HESHIMA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.

AIDHA MHE ABOUD AMELITAKA JESHI LA POLISI KUCHUKUA HATUA ZA KISHERIA KWA WALE WOTE WATAKAOJISHUGHULISHA NA VITENDO VYA UVUNJAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KWANI SIO MAADILI YA WAZANZIBARI.

PIA AMEZIOMBA TAASISI ZA DINI ZOTE KUZIDI KUTOA ELIMU KWA WAUMINI WAO NA WANANCHI ILI KUWAELIMISHA KUHUSU UTUKUFU WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI NA KUWEKA HESHIMA INAYOSTAHIKI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Ankal
    Naomba ufafanuzi, ni lini Zanzibar ikawa ni nchi ya Kiislamu hata kuzuia mikahawa kufunguliwa. Na je watu wengine wajao Zanzibar kipindi hiki ambao si Waislamu watapata wapi huduma ya chakula?.Nakubaliana kabisa kufunga Baa na pia Wanawake kujistiri vyema miili yao na si tu kwa vile ni mwezi wa Ramadhani bali wakati wote kutunza maadili ni vema sana.
    Lakini kufunga mikahawa inanipa shida kidogo, sheria ipi inapaswa kutumika hapa kama anavyoagiza Waziri?

    ReplyDelete
  2. kwa wanaoijua Zanzibar, hilo sio jambo geni. Kama Zanzibar ingekuwa huru kutoka kwenye muungano wangeweza kujitangaza kuwa ni taifa la kiislamu mana zaidi ya asilimia 90 ni waislamu.
    Wanaofungua migahawa na kutembea uchi ni watu wasio na asili ya Zanzibar.Nadhani Waziri Asisitize na kutilia mkazo mila, silka desturi na tamaduni za Zanzibar.
    ANAETAKA AKAE KAMA WAZANZIBARI NA ASIETAKA AONDOKE, BOTI HAIZIDI 20,000 KURUDI WALIKOTOKA.
    MDAU

    ReplyDelete
  3. Hapa Ulaya ni marufuku kuvaa hijabu. jee mtoa maoni no1 unasemaje kuhusu hili ?

    ReplyDelete
  4. hakukuwa na haja ya kutafuna maneno, kama sheria zinakataka, basi utekelezaji unatakiwa muda wote. Kama ni suala la kulinda, mila, silka na utamaduni, inatakiwa Serikali ilinde kwa sheria za nchi. Kauli imetoa kisiasa zaidi kuliko kisheria.
    GNU kuweni wawazi
    mdau

    ReplyDelete
  5. 99% ya watu waishio z'bar ni muslim kwa hiyo migahawa itafunguliwa kila mahala kwa wageni wangapi? aidha watalii wanahudumiwa ktk mahoteli yao ya kitalii na sio ktk migahawa iliyoko karibu na makazi ya watu ambao wote ni muslim. Cha kuzingatia hapo ni kila jamii ina utamaduni wake na mgeni akifika ni lazima aheshimu utamaduni wa wenyeji wake na utamaduni wa wazanzibar ni uislamu na hao wageni ndio wanaouharibu utamaduni mzuri wa uislamu. Hongera waziri pamoja na serikali ya zanziba kwa ujumla kwa kuheshimu mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na utamaduni wa wazanzibar.

    ReplyDelete
  6. Kwa hiyo na KWARESMA nayo iwe hivyo hivyo??????

    ReplyDelete
  7. Kama hivyo ndivyo Waziri anatakiwa awataarifu wahusika kwamba watalii hawaruhusiwi kwenda Zanzibar mwezi wa Ramadhan!

    ReplyDelete
  8. Vitendo viovu ni vya kukemewa hata kama si wakati wa ramadhani. Kauli kama hizi zinaonesha kwamba mwezi wa ramadhani tu ndio mwezi wa kufanya mema halafu miezi mingine ni mtu mwenyewe atakavyojua.

    ReplyDelete
  9. Wewe anony wa kwanza, hupaswi kuhoji mambo ya waislamu. Ninyi ndio watu msiotutakia mema. Watu wenye Fitna kama wewe hatuwataki zanzanibar. Bakini huokhuko kwenu Bara.

    ReplyDelete
  10. Mdau wa kwanza, sheria ya kufunga mikahawa ipo Zanzibar kabla ya mapinduzi. Zanzibar ina wakaazi wengi sana ambao ni Waislam. Sheria za Bara zinazotumika Zanzibar ni chache tu ambazo zimekubalika katika muungano. Wasio waislam wanatakiwa wale ndani ya majumba yao au hoteli za kimataifa ambazo wageni wao sio Wanzanzibari na hata wao hupewa uelewa wa hii sheria. Tatizo kubwa la hii sheria ni kwa ndugu zetu kutoka Bara hawajui sheria za Zanzibar. Ukerewe kuna sheria moja ya "Shouting" ambayo waafrika wengi huwa hawaijui. Matokeo yake huwa wanaivunga bila kujua.

    ReplyDelete
  11. WEWE ANONYM WA KWANZA UNAONEKANA HUJUI CHOCHOTE KUHUSU ZNZ. MAANA KWA WALE WANAOJUA ZNZ WAKATI WA RAMADHANI WASINGEULIZIA SUALA LA MIGAHAWA. HAO WATALII WALIKUA WANAKUJA ZNZ TOKA WAKATI WA KARUME SR, NA WALIKUA WAKIFIKA UWANJA WA NDEGE WANAPEWA SERUNI ZAO HAKUNA VIBUKTA WAKATI WA RAMADHANI NA WALIKUWA WAMELIKUBALI HILO NA KUHESHIMU SHERIA ZA WA ZNZ.MIMI NNAMUUNGA MKONO WAZIRI ASILIMIA 100,NA SI KWA RAMADHANI TU HATA SIKU ZA KAWAIDA VLVL.

    ReplyDelete
  12. "Kwetu ni kwao, Kwao kwetu kwanini".

    Ugly and guff words like, "Kwetu", "Kwao", "Kwangu", "Mimi" , "Wewe", "kwangu" yanaweza kuleta mtafaruku mkuu katika jamii yetu,please try to avoid them especially publicly.

    Mdau
    USA.

    ReplyDelete
  13. Amechemsha inamaana kama si mwezi mtukufu ruhusa kufanya maovu. Hapo ndo watu wafia dini wanakosea, maandiko hayasemi unaruhusiwa kutenda maovu wakati wa siku za kawaida ambazo hatufungi. Ina maana miezi 11 waislamu mfanye dhambi na mwezi 1 kwa mwaka maombi kwa sana. Haya wee hii kali. Mi sioni sababu ya kufunga migahawa kama kila muumini anajua wajibu wake vile zanzibar ni kisiwa cha watalii pia

    ReplyDelete
  14. Mbona marekani hakuna sikuku ya Eid kitaifa, ijapokuwa kuna waislam wazawa?Ukitaka kusali Eid unachukua personal day off bila malipo au ubabatize kwenye vacation/sick days zako, period.
    Ni sherai za baadhi ya sehemu na ni lazima zifuatwe kama unataka kuishi sehemu hiyo.
    Naona ni sawa tu kwa Zbar kuwa na sheria za kulinda utamaduni wao.

    ReplyDelete
  15. Unajua Wadau wa hii Blogu,haya mambo yanashangaza sana,hata kama nchi ni ya kiislamu but hii ni too much sasa. Serikali haina Dini ila kinachoshangaza ni jinsi serikali inavyokazana na udini, sasa hapa waziri(serikali) anakemea uovu kipindi cha ramadhan,mara Rais anafungua chuo cha kiislamu,mara mafunzo ya kiislamu,yani vitu vingi vya kiislamu vinahusishwa na serikali,kwa nini?!

    Waziri na wengine wafanye kazi zao zilizowaweka madarakani na wasitumie nyazifa zao ku-deal na mambo ya Dini. Kwa kweli mi sina tatizo na waislamu ila shida ni jinsi serikali inavyo jihusisha na uislamu ndo nnaposhangaa.

    Mi nlitegemea hayo maonyo na marufuku zote zingekuwa zinatolewa na viongozi wa dini badala ya waziri kutumia wazifa wake na kwa madaraka ya serikali kukemea kidini. Au akemee yeye kama yeye "Muhammed Aboud" na sio kutoa taarifa Rasmi ya serikali kama Waziri.

    Usiibanie hii Ankal,kwa kweli mimi haya mambo ya udini udini- Ukristu,Uislamu,Hindu au Upagani huwa yananishangaza sana hasa kwa nchi kama yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tz.

    Mdau
    Mashariki Ya Mbali Sana.
    (Very Far East)

    ReplyDelete
  16. Nyerere alipokufa ilikua marufuku,sherehe,karamu wala kupiga mziki kwa mwezi mzima ,wadau hapo vipi nayo hiyo ni sheria? so tusichukulie ushabiki jamani viongozi watiiwe hata kama si sheria lakini ni amri.Serikali haina dini mdomoni tu Maana hata nyerere alijidai hilo lakini cha kushangaza cardinali pengo au sijui Cardinali gani aliapishwa uwanja wa amani na wanafunzi kuhudhuria,haya SHEIKH mkuu anachaguliwa na serikali, Tukiangalia nchi tuangalia asilimia ya watu wake,na kuna mdau alosema hijabu ulaya hairuhusiwi ni uongo UK kuna misikiti na mahijabu kama upo Mecca,kisichoruhusiwa ufaransa ni ninja na si hijabu.

    ReplyDelete
  17. unapozungumzia suala la dini, kwa kweli mie linanitatiza sana. kuna kawaida yadini fulani kuona dini nyingine inapendelewa japo kukitajwa kitu kidogo sana. hata mimi nimesha experience hiyo niite chokochoko za kidini. mtu anaweza kusema, kwa mfano, Kikwete kachagua viongozi waislam tupu, ama kafanya hivi kwa waislam;ama ni mdini! bt ukiangalia hicho kinachoambiwa kuwa ni udini, is nothing compared to the reality. I know kuna wanaotamani waamke asubuhi waukute uislamu haupo, but haiwezekani. so tukubaliane na ukweli huo usioepukika. Zanzibar yajulikana wazi kuwa asilimia kubwa ya wakaazi wake ni waislam, therefore hata maadili, sheria na taratibu nyingi ni za kiislam. sasa la ajabu lipi??
    Cha msingi ni kuheshimiana, na kuheshimu taratibu za watu kwa minajir ya sheria zao na mafundisho yao. Basi

    ReplyDelete
  18. Well done SMZ Kwa kuendelea kuulinda utamaduni wa Zanzibar!!!

    ReplyDelete
  19. Sasa kama suala ni watu wengi ni waislamu, mbona kule bara mnataka kulazimishia mahakama ya kadhi iingizwe kwenye mambo ya serikali wakati kijua bara kuna wakristo wengi? Mlishaambiwa kama manataka mahakama ya kadhi ruksa lakini muianzishe na kuiendeleza ninyi wenye dini hiyo mkakataa. Kisa mnataka serikali iwabebe. Kwa hiyo hata kodi za wakristo zikatumike kuendeshea mahakama ya kadhi?

    ReplyDelete
  20. wenye chuki na uislamu MUNGU atawashinda, ukienda kwa machongo jicho lako moja ulifunge!kukitajwa jambo linalohusiana na uislamu watu hawapendi wanaumia sana.WHY?

    ReplyDelete
  21. Mimi nakubaliana na kauli ya waziri ,lkn tatizo langu ni moja ....huku zanzibar kuna wakristo ambao wanafanya kazi za serikali pia na wengine wanasaidia taasisi mbalimbali lkn sio wakazi kwa maana wamekuja kwa muda tu....mimi nikiwa mmoja wapo...sasa watu kama hawa ambao wanawasidia wazanzibari kitaalamu pia wale wapi wakati wa mchana na asubuhi.....ushauri ni kwamba serikali ingeruhusu sehemu maalum tu moja au mbili kutoa hizo huduma na nyingine kufungwa ili kusaidia hawa wachache ambao wanafanya kazi huku kwa muda lkn sio waislamu.

    Yangu ni hayo tu.....

    ReplyDelete
  22. si suala la sheria bali serikali ina uwezo wa kutoa amri kukemea na kufanya lolote kama nyerere alipokufa ikawa marufuku sherehe yoyote,sasa hiyo ni amri mbona xmass jamani askari wanakua wengi mitaani je na wao ni wadini? kila kona ya mji utakuta askari kulinda usalama hiyho ni amri tu jamani si suala la dini,wengi wape

    ReplyDelete
  23. MI NADHANI NASHERIA YA BAKORA INGETUMIKA KWA WOTE WANAOVUNJA MAADILI YETU MAANA UTAONA MTU MZIMA NA AKILI YAKE KAVAA KITAIT RAMADHANI HII ANATIKISA MATAKO HATA HAYA HAONI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...