Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akipata maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Jain Irrigation System ya India Bwana Anirudha Barwe namna umwagiliaji wa matone wenya gharama nafuu unavyofanya kazi kwenye Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima, Nane Nane katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma leo.

Na Issa Sabuni, WKCU

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe leo alitembelea Banda la Kampuni ya Jain Irrigation System ya nchini India na kujionea namna Kampuni hiyo ilivyojipanga katika kuwawezesha wakulima wa Tanzania ili watumie teknolojia mbalimbali za kilimo cha umwagiliaji.

Katika banda la Kampuni ya Jain Irrigation System, Waziri Maghembe alionyeshwa teknolojia ya umwagilijai wa kusambaza mipira juu ya shamba “surface irrigation”, umwagiliaji wa kunyunyizia “overhead/sprinkler irrigation” na wa kupitisha mipira na mabomba chini ya ardhi “sub surface irrigation”.

Waziri Maghembe alimweleza Mwakilishi mkazi wa Kampuni hiyo Bwana Anirudha Barwe kuwa mpango kabambe wa Taifa wa umwagiliaji unalenga kulifanya taifa lijitosheleze kwa chakula na kuongeza kuwa hekta milioni 29.4 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji huku hekta milioni 2.3 zina uwezo mkubwa wa kuendelezwa na hekta milioni 4.8 zina uwezo wa kati wa kuendelezwa.

Waziri Maghembe aliongeza kuwa licha ya changamoto zilizopo Serikali imeimarisha kilimo cha umwagiliaji nchini kwa kuongeza eneo linalotumiwa kwa kilimo cha umwagiliaji kufikia hekta 345,690 katika skimu za umwagiliaji 2,006 zilizosambaa mikoa yote nchini.

Aidha, Waziri Maghembe alimweleza mwakilishi huyo kuwa azma ya kukifanya kilimo cha Tanzania kuwa na tija na manufaa kwa mkulima wa Tanzania ni kazi ya Serikali na wadau wengine kama Jain Irrigation System.

“Lengo la Serikali si kujitosheleza kwa chakula tu lakini pia kuhakikisha kuwa mkazo unaongezwa katika kuzalisha mazao yenye thamani kubwa kama mboga na matunda na tutafanikiwa kama wakulima wataitumia rasilimali maji ipasavyo.” Alikaririwa Waziri Maghembe.

Aliongeza kuwa kilimo cha umwagiliaji kina tija kubwa kama rasilimali maji itatumika ipasavyo sambamba na teknolojia nyingine za kilimo bora na kutolea mfano Jimbo la Andhra Pradresh linavyozalisha ndizi za kutosha soko la ndani la India na la dunia na kuifanya nchi hiyo kuwa mzalishaji wa kwanza duniani.

Aidha, Waziri Maghembe alifurahishwa unafuu wa bei za Kampuni hiyo kuanzia wakati wa kuandaa shamba na hatmae kufunga miundombinu na mitambo ya kilimo cha umwagilijai lakini alimwomba Mwakilishi mkazi wa Kampuni hiyo kuendelea kumfiria mkulima mdogo ili kumpa unafuu zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Wasomi wa SUA mpo wapi ,hivi hatuna hata wataalam wa umwagiliaji mpaka tuwatoe India! Angalieni hicho kibomba cha maji eti cha bei nafuu.
    Tuache siasa na tutumie elimu zetu kujikwamua kwani hawa tunao wategemea wamesoma kama sisi ila sio wavivu wa kufikiri, tutasadiwa mpaka lini?

    ReplyDelete
  2. Kweli bongo unakwenda na briefcase na kuondoka tajiri

    ReplyDelete
  3. Sisi ni wavivu wa kufanya kazi na hata kufikiri pia,acheni watu wafanye kazi msiwaonee gere sababu ni wahindi. Ni kawaida watu wa far east ni wachapa kazi mno.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...