Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Productions Ltd inayoendesha shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011 (BSS) Rita Paulsen akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip jijini Dar, kwa madhumuni ya kuwatambulisha wadhamini wapya wa shindano hilo,ambao wanatambua na kuthamini vipaji vya Tanzania,Wadhamini hao ambao pia watahakikisha BSSsecond Chance 2011 inachukua sura mpya kwa Watazamaji.Ritha amewataja wadhamini hao kuwa ni kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, PSI (Salama Condoms),CHAMPION (Engender healt),NSSF na Golden Tulip Hotel.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Productions Ltd inayoendesha shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011 (BSS) Rita Paulsen akitaja washiriki waliofanikiwa kuingia kumi bora,kama waonekavyo nyuma pichani ambao ni Rogers Lucas (23),Bella Kombo (5),Chibi Dayo (7),Sarafina Mshindo (12),Hajji Ramadhan (11),Mary Banyukwa (15),Mary Lucos (16),Waziri Salum (27),Beatrice William (4) pamoja na Iman Lissu (12).
Pichani kulia ni Mwakilishi kutoka NSSF,Theopiste Mhata,Meneja Masoko PSI (salama condoms),Robinson Katule,na shoto ni Muwakilishi wa hoteli ya Golden Tulip,Sharon Evelyn pamoja na Afisa viwango wa Tigo,Pamela Shelukindo.
Aidha Rita aliongeza kusema kuwa kama kawaida ya kampuni ya Benchmark kila mwaka inaongeza dau la zawadi ili kuboresha na kubadilisha maisha ya washiriki,"Mwaka huu jumla ya shilingi milioni 55 zitashindaniwa na washiriki",alisema Rita paulsen.

Bongo Star Search Second Chance 2011 (BSS) hurekodiwa Mbalamwezi Beach Club na kurushwa hewani na kituo cha televisheni ITV siku ya jumamosi kuanzia saa 3:00 usiku na kurudiwa siku ya jumanne saa 5:00 usiku.
Pichani washiriki kumi bora waliofanikiwa kuingia kwenye shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011 (BSS) .
Pichani washiriki kumi bora waliofanikiwa kuingia kwenye shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011 (BSS) .

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...