Sehemu ya majengo ya Machinga Complex yaliyoko eneo la Ilala, Dar es salaam.

Akifanya majumuisho ya ziara yake ya kukagua jeng hilo , Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Dkt. Masabuli,  aliagiza kuwa vyumba vyote vya biashara (vizimba) vilivyogawiwa kwa wafanyabiashara bila  utaratibu virejeshwe kwa bodi mpya ya jengo hilo na shughuli ya ugawaji ifanyike upya. Pia aliagiza kuwa vizimba 344 vilivyogawiwa kwa wafanyabiashara katika jengo hilo ambavyo havitumiki vigawiwe upya.Aliagiza kutolewa kwa nyavu zilizotumika kwa ajiri ya kutengenisha vizimba ndani ya jengo hilo kwani vimewekwa pasipo kuzingatia umuhimu ya mahitaji kwa watumiaji.  Nyavu hizo zilinunuliwa na kutengenezwa kwa thamani ya shilingi Bilioni 1.2
Meya wa jiji la Dar es salaam Dkt Didas Masaburi akitembelea majengo ya Machinga Complex jijini Dar es salaam. 
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dkt Didas Masaburi, akikagua moja ya vizimba ndani ya jengo la Machinga Complex 
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masabuli, aizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea jengo la Machinga Complex jana asubuhi. 
Meya wa jiji la Dar es Salaam Dkt. Didas Masabuli,akizungumza na waandishi wa habari  kwenye jengo la Machinga Complex jijini Dar es Salaam alipotembelea kukagua vizimba vya wafanyabiashara.
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masabuli akizungumza na akina mama wauza Batiki wanaofanya biashara hiyo pembeni ya jengo la Machinga Complex kutokana na kukosa nafasi ndani ya jengo hilo.Masaburi aliuagiza uongozi wa jengo hilo, kuwapatia nafasi akina mama hao haraka.
Waandishi wa habari wakiwa katika msafara na Meya wa ´jiji   ndani ya Jengo la Machinga Complex jana asubuhi. Picha Zote na Mdau Victor Makinda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hizo cages ni za nini? au za kufugia kuku? Kwa nini mazingira yasiboreshwe, yawe ya kuvutia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...