Katika kituo cha Daladala cha Kinondoni Studio leo majira ya mchana hali ikuwa hivi mara baada ya daladala mbili zenye route tofauti kupigana pasi kutona na uzembe wa uegeshaji mbaya wa daladala hizo na kupelekea hali kuwa maka hivi.daladala nyingi za jijini Dar hazipendi kuegesha na kupakia abiria katika vituo husika hali inayopelekea kuleta usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara au kutokea kama haya yaliyotokea hapa.
Abiria wakilazimika kushuka kwenye moja ya madaladala hayo baada ya kuona mambo hayaeleweki kutokana na pasi hilo.sijui ni jitihada gani za lazima zifanyike ili kutokomeza kabisa hali hii??
Kubenea amlalamikia Manji
ReplyDeleteNa Muhibu Said
2nd August 2011
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, Saed Kubenea, amewasilisha malalamiko kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akimuomba kuingilia kati mwenendo wa kesi iliyoamuliwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke dhidi yake, kwa kusikiliza upande mmoja tu wa mfanyabiashara, Yusufu Manji.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Manji dhidi ya Kubenea, Mhariri wa MwanaHALISI, Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers Limited na Printech Company Limited, Julai 18, mwaka huu.
Kubenea amewasilisha malalamiko hayo kwa niaba ya wadaiwa wenzake kupitia barua yake kumbukumbu namba. HHPL/ADM/1101 ya Julai 25, mwaka huu, yenye kichwa cha habari: “Malalamiko dhidi ya kesi ya madai Na. 43/2011”.
Anadai Manji aliiomba mahakama itoe amri kwa kusikiliza upande wake mmoja tu na mahakama ilifanya hivyo na kuamuru.
Amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Rose Kangwa, Julai 19, mwaka huu, inawataka kuwasilisha kwa Manji hati ya viapo vyao, nyaraka zote za asili na vivuli, walizonazo zinazohusu taarifa anayolalamikia katika gazeti la MwanaHALISI, toleo namba. 250 la Julai 13-19, mwaka huu na kueleza walikozipata.
Kubenea anadai pamoja na kuwasilisha hati ya madai ya msingi siku hiyo, Manji alifungua pia maombi ya zuio siku hiyo hiyo. Anasema si kawaida maombi ya zuio la dharura kusikilizwa kwa njia hiyo kama alivyofanya hakimu huyo.
Anadai hati ya madai na amri ya zuio ya mahakama, vilipelekwa ofisini kwake Dar es Salaam siku hiyo hiyo ya Julai 19, akiwa Dodoma kusaka habari za Bunge linaloendelea hivi sasa.
“Wakati huo, mimi binafsi, ofisi yangu na hata wadaiwa wengine hatukuwa na taarifa zozote za kuitwa shaurini. Tunatishika kwa hatua ya Hakimu wa Mahakama Temeke kupanga na kukubali kusikiliza maombi ya mdai haraka kiasi hicho bila kutaka tujulishwe, bila kutaka tuhudhurie na bila kutaka tusikilizwe,” anasema.
Anasema ofisi yake na za wadaiwa wenzake ziko Dar es Salaam na zinafikika na kwamba, urahisi wa kuzifikia umedhihirika kwa jinsi Manji alivyofaulu kufikisha kwao ‘mara moja’ amri ya mahakama.
Kwa kuzingatia hayo, anasema walinyimwa haki ya kusikilizwa na utaratibu uliotumika una sura ya kinyemela.
Anasema kwa hayo yanayotokana na matakwa ya Manji na yaliyokubaliwa na mahakama hiyo bila kuwapo kwake, wakili wake wala wadaiwa wenzake, ni wazi kuwa wananyang’anywa haki ya kujibu na kutishiwa bila kusikilizwa.
Pia wanaonyeshwa kana kwamba kumekuwa na kesi na sasa imeisha, hivyo wanapewa masharti na mahakama, wanashinikizwa kufichua vyanzo vya habari vya gazeti kwa maslahi binafsi, kabla kesi haijasikilizwa na mahakama kuamua iwapo kuna sababu ya kufanya hivyo “kwa maslahi ya umma.”
“Mimi binafsi na wadaiwa wenzangu, tuna imani na mahakama. Kwa msingi huo, ninakusihi uingilie kati mapema iwezekanavyo, mwenendo wa kesi husika, kwa kuitisha jalada la kesi yenyewe ili ulipitie na kulifanyia maamuzi,” anasema.
CHANZO: NIPASHE
mambo hayo wababe wenyewe wamekutana .kila mara wanawaonea wadogo.
ReplyDelete