Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein akitoa ushauri juu ya upandaji wa Miche ya Mikarafuu katika kitalu kilichopo Chake Chake Pemba. kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Zanzibar, Afan Othman na Kushoto ni Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui ambapo usoni kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Meja Mstaafu Juma Kassim Tendwa.
Rais Shein akichuma karafuu kuashiria uzinduzi rasmi wa uchumaji wa Zao hilo katika Msimu huu huko Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein akipima karafuu katika uzinduzi wa Uchumaji wa zao hilo huko Mkanyageni Pemba.
Rais wa Zanzibar Dk. Shein akichambua karafuu katika siku ya uzinduzi wa Uchumaji wa Zao hilo Mkanyagei Pemba, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC)
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein akianika Karafuu pamoja na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui katika siku ya uzinduzi wa Uchumaji wa zao hilo Msimu huu huko Pemba.
Rais Dk. Shein akitoa ufafanuzi juu ya upimaji wa karafuu usoni kwake ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui
nakupongeza kwa website yako, naomba nitumie namba yako ya simu katika simu yangu.
ReplyDeletendugu yako Haruna Chambika ( TRL )