Meneja Biashara na Masoko wa Kampuni ya Real Insurance,Amani Boma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakuitambulisha huduma yao mpya kwa jamii ya Amani Motor Insurance Policy katika hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kampuni hiyo,iliyopo PPF Tower ghorofa ya pili.kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo,Stephen Okundi na kushoto ni Mhasibu Mkuu wa Kampuni hiyo,Thecla Mangashi

KAMPUNI ya Real Isurance ya jijini Dar es salaam,leo imezindua huduma ya kipekee ya bima iitwayo Amani Motor Insurance. Huduma hiyo ambayo ni ya kipekee itamwezesha mteja kuwa na Amani kama jina la bima hiyo lilivyo. Hii ni kwa sababu huduma ya bima inayotolewa na kampuni hiyo itamfanya mteja aliyepata ajali aendelee na shughuli zake bila wasiwasi wakati kampuni hiyo itakuwa inamuhakikishia usalama wa gari lake.

Faida za Amani ziko nyingi na nzuri ikiwa ni msaada wa pesa ya usafiri kwa muda usiozidi mwezi mmoja kwa kuzingatia vigezo na masharti ya bima ya Amani .Mteja atapewa msaada huo wa usafiri wakati gari lake liko kwenye matengenezo katika gereji zilizothibitishwa na kampuni ya REAL Insurance,Kama mteja hakuwa mwenye makosa na hakusababisha ajali, kampuni ya REAL Insurance itamwondolea ada ya lazima kwa ajali iliyotokea,Uvutaji bure wa gari lilopata ajali mpaka gereji au kituo cha karibu cha Polisi,Matibabu kwa mtu wa karibu (mke au mume) mpaka na watoto watatu watakaokuwepo kwenye gari wakati wa ajali.

Kwenye bima hiyo ya Amani, mteja atafanyiwa uthamini wa gari lake bila malipo yeyote ya ziada kabla ya kukata bima.

Vigezo na masharti ya huduma hiyo ni muhimu kuzingatiwa kama vile ni lazima gari liwekewe bima kubwa (Comprehensive ) na ni lazima gari liwe na thamani isiyopungua Shs 10, 000, 000 (Milioni kumi) na kuendelea.

Ufahamu wa bidhaa za bima bado ni changamoto kubwa sana na jamii bado inahitaji uelewa zaidi juu ya sekta ya bima na uendeshaji wake. Athari yake imeonekana kote ndani na nje ya makampuni ya bima.

Kampuni hiyo ambayo imejikita katika kuhakikisha inakuwa ya kisasa zaidi kupitia ubunifu na uharaka wa kutimiza matarajio ya wateja kwa kuweka mazingira mazuri zaidi ya kiutendaji na kibiashara na bado inaendelea kutafuta njia mbadala za kuboresha huduma kwa wateja wetu ili kutatua changamoto zinazokabili utendaji katika biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...