MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu (PICHANI) ,amehenyeshwa kwa kuhojiwa kwa undani na Baraza la Mawaziri kuhusu kuyumbisha bei ya mafuta.

Baraza hilo lilitaka kujua kwa nini mamlaka hiyo imekuwa ikiyumbisha nchi na wananchi kuhusu bei za mafuta.

Kwa zaidi ya saa moja, Masebu na wasaidizi wake waliwekwa kiti moto kuhusu bei zilizotangazwa na Ewura mwishoni mwa wiki, ambazo zimepanda kwa asilimia sita kutoka zile zilizotangazwa awali.

Habari za kuaminika kutoka kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, mjini Dodoma zinasema kuwa waziri mmoja baada ya mwingine walimhoji Masebu na wasaidizi wake kuhusu mwenendo usioridhisha wa bei za mafuta nchini.

Habari zinasema kuwa Masebu ambaye aliingia kwenye ukumbi huo akionesha kujiamini, alianza kupoteza mwelekeo kwa kadri maswali yalivyokuwa yakimiminika kutoka kwa mawaziri.

Hatimaye siyo yeye mwenyewe ama yoyote kati ya wasaidizi wake ambaye alikuwa na majibu ya kutosheleza ama hata ya kuwashawishi mawaziri kuhusu hatua hizo za Ewura na kwa kadri kikao hicho kilivyoendelea, Masebu na wenzake walionekana kukosa hoja.

Habari zinasema kuwa Masebu na wasaidizi wake walitakiwa kujielezea mbele ya Baraza la Mawaziri ili kuliwezesha Baraza hilo, chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kujiridhisha na mwenendo mzima wa bei mafuta.  


Chanzo na Habari zaidi nenda Habari Leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nyie EWURA mlipokomaa na hao wanafanyabiashara wa mafuta tulijua mna meno na yanayong'ata haswa, na siyo ya plastic. Lakini kwa hili la kupandisha bei ghafla bin vuu imeonyesha hata hayo ya plastic hamna, ni vibogoyo tu...

    ReplyDelete
  2. Wanatumika kisiasa ili ionekane serikali haifai na kuleta vurugu za kisiasa nchini,Masebu atolewe ni msalitiWanatumika kisiasa ili ionekane serikali haifai na kuleta vurugu za kisiasa nchini,Masebu atolewe ni msaliti

    ReplyDelete
  3. Huu ni upotoshaji kabisa!! EWURA inatumika kupotosha umma sababu kazi yake si kupanga bei ya mafuta bali ni kusimamia shughuli nzima ya nishati Tanzania. Katika soko huru au huria "Free Market" bei hupangwa na Soko na sio maofisa waliokaa katika chumba cha kiyoyozi. EWURA pamoja na tume ya ushindani"Competition commission" kama ipo kazi yake ni kuhakikisha soko ni huru na hivyo kupambana na ukiritimba, au wauzaji kushirikiana kupanga bei.
    EWURA na Serikali hawana mafuta, hawanunui mafuta na hawajui nini gharama ya kampuni inaingia sasa inapanga bei kwa kutumia kigezo gani?!
    Tanzania hatuwezi kutafuta bei zetu rahisi kilichopo ni serikali kuangalia mfumo mzima wa bei na kama inataka kuwasaidia wananchi basi ipunguze KODI kwenye bei na sio kuwaonea watu binafsi.
    Kuwapangia bei makampuni ni sawa na KUTAIFISHA MALI na pia ni kinyume cha katiba ambayo inamtaka mtu kulipwa fidia halali ya mali yake.
    Kulazimisha bei ni kuahirisha tatizo maana hawa jamaa wakishindwa kuagiza mafuta tatizo litakuwa MARADUFU.
    Tusidanganyane kwa kutumia AMRI tuwe makini, tutumie busara na TUJENGE SIO TUBOMOE KATIKA KUJENGA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...