Mwenyekiti wa bodi ya benki ya Exim Tanzania Yogesh Manek (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu foram ya siku moja ya menejimenti ya benki hiyo iliyowajumuisha Wakurugenzi wote wa bodi  na Mameneja wa matawi yote nchini iliyokutana Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kutathimini utatendaji wa benki hiyo.Kushoto ni Meneja Mkuu wa benki hiyo Dinesh Arora na katikati ni Meneja Masoko na Uhusiano Linda Chiza.
 Mwenyekiti wa bodi ya benki ya Exim Tanzania Yogesh Manek (kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya washiriki wa foram ya siku moja ya menejimenti ya benki hiyo iliyowajumuisha Wakurugenzi wote wa bodi  na Mameneja wa matawi yote nchini iliyokutana Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kutathimini utendaji wa benki hiyo.

Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Exim imeendelea kujijenga na sasa imeazimia kuongeza faida yake na kufikia Sh. bil 18/- ifikapo mwisho wa mwaka huu ikitoka katika rekodi ya faida ya sh. bil 14/- ya mwaka 2010.

Meneja Mkuu wa benki hiyo Dinesh Arora aliyasema hayo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika foram maalumu ya menejimenti ya benki hiyo iliyokutana kutathimini utendaji wa benki hiyo.

Alisema pamoja na mafanikio makubwa ya kiutendaji ndani ya benki hiyo tangu kuanzishwa kwake bado menejimenti imeona kuna umuhimu wa kukutana na watendaji wakuu wa benki hiyo na kutathimini jinsi ya kujijenga zaidi.

Foram hiyo ya siku moja iliwahusisha Wakurugenzi wote wa bodi ya benki hiyo pamoja na Mameneja wa matawi yote nchini wakiaamini mkusanyiko huo utaweza kutoka na mikakati mipya itakayohakikisha benki hiyo inakuwa mara dufu ya ilipo sasa.

“Ni jambo la kujivuna kwetu kwani tumekuwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwa utendaji wa benki hii ambapo sasa tumezamiria kufikia faida ya bilioni 18/- itakapofika mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni hatua kubwa ukilinganisha na bilioni 14/- za mwaka 2010.

“Pamoja na mafanikio hayo, menejimenti imeona kuna haja ya kukutana kama timu moja na watendaji wote wa benki yetu katika kuangalia jinsi ya kusonga mbele kwa kutathimini mahali tulipo na tunakusudia kufika wapi na ili tufike huko tufanye nini?”, alisema Arora.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Yogesh Manek alisema ni foram ya kuijengea uwezo zaidi timu ya menejimenti yetu katika kuongeza ufanisi wa kiutendaji.

Alisema benki hiyo imekuwa na maendeleo makubwa lakini bado wana changamoto kadhaa zinazowakabili hivyo hawana budi kukutana na kutathimini kwa jumla na kutoka na mikakati yenye tija itakayowasaidia kusonga mbele.

“Popote penye maendeleo lazima patakuwa na changamoto ambazo kama watendaji tunapaswa kuzitathimini na kuzipatia ufumbuzi, kiujumla tumekutana tupate mawazo ya pamoja ya jinsi tunavyoweza kupiga zaidi hatua”, alisema Manek.

Benki ya Exim Tanzania inayojumuisha wanahisa Wazalendo ilianza kutoa  huduma zake mwaka  1997 ikiwa na tawi moja Dar es Salaam katika mtaa  wa Samora ambapo sasa imeweza kupiga hatua kubwa ikiwa na matawi  kadhaa nchini na nje ya nchi.

Benki hiyo sasa ina matawi 21 yanayotoa huduma kamili za kibenki  katika maeneo mbalimbali nchini ambapo pamoja na mengine Dar es Salaam  kuna tawi la Ofisi Kuu, Clock Tower, Samora, Mlimani City, Temeke, Namanga, Kariakoo, Ubungo, na Nyerere.

Matawi mengine nje ya Dar es Salaam ni Tanga, Zanzibar,Mtwara, Arusha, Mount  Meru (Arusha),Morogoro, Mbeya,  Mwanza, Moshi, Babati, Iringa na Karatu  pamoja na nchi za nje yaliyopo Comoro ambayo ni Moroni na Anjouan na moja lililopo Djibouti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tanzania tulikuwa na mabenki mengi ya umma ambayo faida ilikuwa inakwenda hazina na kunufaisha sekta nyengine. Sasa hawa EXIM wanachukua hiyo faida na kupeleka kwao Canada na Pakistan kuendesha maisha yao na jamaa zao!!
    Mdau
    Bado Mjamaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...