Mkazi wa jijini Dar es Salaam akipita mchana huu mbele ya kituo cha mafuta cha BP kilichopo mtaa wa Makunganya na Mkwepu jijini Dar es salaam ambacho kimefungwa tangu serikali itangaze bei mpya ya mafuta. Uchunguzi uliofanywa katika baadhi ya vituo umeonyesha kuwa vituo vingi bado vipo katika mgomo baridi kwa kisingizio cha kuishiwa wese. Tayari EWURA imetoa tadhadhari kwa wafanyabiashara wqanaojifanya kichwa ngumu na wenye jeuri ya pesa kwamha serikali haitosita kumchukulia hatua yeyote atayekaidi agizo halali ya wese kuuza kwa bei halali iliyowekwa.  Picha na Francis Dande




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. HII NI TABIA CHAFU TENA SHIRIKA KAMA BP???? ICHUKULIWE HATUA KALI HAWA WATU PESA ZOTE WANAZOPATA HAWAWEZI KUWAFIKIRIA WANANCHI HATA MIEZI 6??? KZ

    ReplyDelete
  2. TUMESHAZOEA MATAMKO YA SERIKALI YASIYOOGOPEKA KWA WENYE PESA, TABU NI KWA SISI WALALA HOI TU...lakini nadhani umefika muda wa serikali kuangalia upya hili suala la biashara huria maana linatutafuna mno sisi wananchi wa hali ya chini kimaisha. serikali ifike mahali pa kuamua kurudi kulekule kwa kuagiza mafuta yenyewe na kuuza kwa manufaa yake na pia kwa kuwahurumia wananchi wake.vinginevyo naona hii ni danganya toto tu, serikali na hao wenye pesa wanajuana maana usishangae hao ndio wanaoishikilia serikali ndo maana hawaogopi hata llikitoka tamko la aina gani...HAO KIBOKO YAO ALIKUWA MUASISI WA TAIFA LETU AMBAYE HAKUWA NA HAYA KWA WALAFI NA WAHUJUMU UCHUMI, WASIOKUWA NA HURUMA KWA WANANCHI WENYE VIPATO VYA CHINI...ipo siku tu kama serikali imeshindwa itasaidiwa, muda utafika tu...mimi ndo naamini hivyo siku zote kila kitu kina mwisho, ni vyema serikali kuzima hizo cheche kabla moto hujawa mkubwa maana hapatakuwa na hiyo amani wanayoiona na kuimba kuwa ni ya kudumu

    ReplyDelete
  3. Hii inaitwa JARIBU PIGA MIMI TAONA GUVU YANGU kumbe hamna lo lote.

    Tangu wiki iliyopita Serikali inatoa matamko, mara inazungumza na wenye mafuta lakini ni wachache tu ndiyo walioitikia mwito huo. Jee ikifika jumanne siku ya kazi itakuwaje?

    EWURA fanyeni uamuzi mgumu siyo kutukamua sisi wananchi kwa kuchukuwa asilimia tatu na kuvimbisha matumbo yenu.

    ReplyDelete
  4. Serikali/EWURA ndio muda wa kufanya maamuzi Magumu sasa bila kuogopa!

    ReplyDelete
  5. Wenye vituo vya mafuta ndio serikali(wabunge na mawaziri) jamani,hivi mnafikiria kutafanyika nini?

    ReplyDelete
  6. Dawa tu ni kuiondoa hii serikali inayoshirikiana na mafisadi ifikapo 2015. Ni kipindi kama hiki ambapo wengi wetu tunamkumbuka Mwalimu Nyerere.

    ReplyDelete
  7. Hao BP sio huko Dar peke yake, hata huku Dodoma hawauzi mafuta kabisa toka hiyo siku, kwa kweli inasikitisha....Labda kwa sababu Viongozi wa Serikali wao mafuta ya magari yao yanachukuliwa kwenye Bohari za Serikali na kwenye vituo walivyoviteua...Lets pray.

    ReplyDelete
  8. EWURA ni mbwa koko, anabweka saaana lakino matendo hakuna! Yaani ukiniambia kuna serikali toka mgomo huu uanze, mie hata siamini! Yaani wiki karibu mbili sasa hatupati mafuta, halafu business as usual? Kweli serikali yetu ni legelege!

    ReplyDelete
  9. Anony wa sita: Una mawazo mazuri, lakini Wa-TZ tu wepesi sana kusahau. Utaona hiyo 2015, watu wanaolalamika sasa hivi watavaa mashati na kofia za rangi ya kisamvu. SUBILI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...