Wadau waliokula nondozzz katika mahafali ya tano ya kozi maalum ya teknologia ya ushirikiano baina ya chuo hicho na cha India, Avinashillingham Deemed.

Na Francis Dande
DUNIA inahitaji watu wenye wenye uwezo na taalum bora ya teknologia ili kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya teknologia, kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta wakati wa mahafali ya tano ya kozi maalum ya teknologia ya ushirikiano baina ya chuo hicho na cha India, Avinashillingham Deemed.

“Pamoja na kasi ya mabadiliko na ugunduzi mpya katika teknologia, tunaweza kukiri kwamba teknologia inaipeleka dunia kwenye mwisho usiofahamika, hivyo dunia inahitaji hao ili kwenda sambasamba na mambo hayo”alisema.

Alisema licha ya teknologia kukua kwa kasi, bado kuna pengo kubwa kati ya ujuzi wa teknologia na mahitaji katika viwanda, ambapo anaamini kwamba wahitimu hao waliobobea kwenye fani husika watakuwa daraja la kuziba pengo husika.

Awali Makamu wa chuo cha India, Kanali Prof. Sheela Ramachandran alisema chuo chake kimekuwa na ushirikiano na IFM kwa malengo mbalimbali likiwemo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya utawala na teknologia.

Alisema wataendelea kushirikiana na IFM ili malengo husika yafikiwe na kuzalisha wanataaluma wenye uwezo wa kwenda sambasamba na mabadiliko ya dunia.

Alisema watu wa sasa hawahitaji fursa ya kupata elimu ya juu bali fursa za kuweza kupata elimu ya juu bora kwa gharama nafuu. Aliongeza gharama kubwa hazitakuwa na maana kama hakuna jitihada za kutoa elimu bora na nzuri.

Katika mahafali hayo wanafunzi 45 walitunukiwa vyeti katika kozi ya utawala na teknologia. Vyuo hivyo vilifikia makubaliano ya kuwa na uhusiano na kutoa kozi hizo mwaka 2006 ambapo tangu kufikiwa yameonyesha maendeleo makubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera kwa wote mliohitimu maana sasa ndio mda wenu wa kufanya ubunifu wa yale mliojifunza .Kumaliza elimu si kuwa na karatasi(vyeti) ila ni kutumia elimu kujikwamua kwenye hizi shida zetu za kila siku.
    Tuna wasomi wengi sana ila wote wamehamia kwenye siasa na kuacha waliojifunza hatimae tunaishia kutegemea kila kitu kwa wachina tena vitu vyenyewe ni kiwango cha chini sana .
    Kazi kwenu kutumia maarifa na ujuzi mliopata tujikomboe na kuikomboa nchi yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...