Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya kukoboa kahawa ya Tanganyika,(TCCCo)Maynard Swai akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya mpango wa kuuza sehemu za mali zake kwa ajili ya kukinusuru kiwanda cha kahawa.
 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya kukoboa kahawa ya Tanganyika,(TCCCo)Maynard Swai akizwaonesha wanahabari baadhi ya mitambo ya kukobolea kahawa ambayo inadaiwa kukoboa kahawa chini ya kiwango.
 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya kukoboa kahawa ya Tanganyika,(TCCCo)Maynard Swai akiwatembeza wanahabari kuangalia baadhi ya mitambo ya kukobolea kahawa ambayo inadaiwa kukoboa kahawa chini ya kiwango.
 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya kukoboa kahawa ya Tanganyika,(TCCCo)Maynard Swai akizwaonesha wanahabari baadhi ya mitambo hiyo.
Wafanyakazi i wa kampuni ya kukoboa kahawa ya Tanganyika,(TCCCo) wakiwa kazini wakati wa ziara hii

Picha na Habari na  Dixon Busagaga, 
wa Globu ya Jamii, Moshi.

BODI ya kampuni ya kukoboa kahawa ya Tanganyika (TCCCo) imelazimika kuuza sehemu ya mali zake ili  kukinusuru kiwanda cha kukoboa kahawa na madeni yanayokikabili baada ya kupata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 2.
Hatua hiyo inafuatia baada ya bodi kuelezea kupungua kwa kiwango katika ukoboaji wa kahawa kiwandani hapo ikilinganishwa na ukubwa wa mitambo ambayo pia imeelezwa kuwa ni chakavu.  
 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni hiyo, Maynard Swai alisema  hali hiyo pia imechangiwa na baadhi ya wanahisa wa kampuni hiyo waliokuwa wanakoboa kahawa yao kiwandani hapo kusitisha kukoboakwa maelezo ya kushuka kwa ubora wa kahawa yao. 
 Alisema pamoja na sababu hizo, pia kuwepo kwa watu binafsi wanaokoboa kahawa nchini, pia kumeathiri zoezi la ukoboaji wa kahawa katika kiwanda hicho ambacho awali kilijengwa kwa madhumuni ya kukoboa kahawaya nchi nzima..Swai alisema hatua hiyo imeilazimu bodi kutafuta njia madhubuti zitakazochukuliwa ili kukabiliana na  changamoto zinazo kikabili kiwanda ili ziendane na mabadiliko yaliyojitokeza baada ya kushuka kwa uzalishaji wa kahawa nchini. 
Swai alisema bodi imeazimia kununua mtambo mmoja wenye uwezo wa kukoboa tani sita za kahawa ya maganda kwa saa moja ambapo tathmini za awali zimeonyesha kuwa mtambo huo unapatikana kwa gharama nafuu. “Tunategemea kununua mtambo kutoka kampuni moja ya Pinhalense ya Brazil,kwa gharama ya dola 686,538 hili litafikia lengo la kuhamasisha wakulima wadogo wa kahawa ambao ndio walengwa wa TCCCo, kurejesha kukoboa kahawa yao kiwandani hapa”alisema Swai.  
Swai alisema tathmini iliyofanywa ilibainisha kuwa mashine hizo pia zimefungwa katika viwanda vyote hapa nchini, ambapo zimesaidia kupunguza gharama za uendeshaji. Alisema katika kufanikisha ununuzi wa mitambo hiyo bodi ya wakurugenzi ya kiwanda hicho imeamua kuuza nyumba tatu zinazomilikiwa na kiwanda hicho, ili kupata kiasi cha shilingi bilioni 1.32 za ununuzi wa mtambohuo.  Hata hivyo Swai alisema bodi ya TCCCo imelazimika kutoa ufafanuzi huo kufuatia kufuatia minong’ono iliyozagaa kuwa, kampuni hiyo inataka kuuza mali zake kwa njia ya ufisadi na kwamba  hakuna uhalali wowotewa kuuza mali hizo  kwani zingetumika kama dhamana kukopa fedha benki.Swai alisema ingawa TCCCo inamilikiwa na vyama vikuu sita vya ushirika lakini bodi ya wakurugenzi wake inajiendesha chini ya sheria ya kampuni.“Yapo maneno mengi mtaani ya kwamba KNCU inauza mali zake, kusema hivi tunakosea, si sahihi hata kidogo…TCCCo iko chini ya sheria ya kampuni, hivyo basi bodi ina mamlaka kamili ya uamuzi kama kampuni,” alisema Swai.Swai alisema mali zitakazouzwa ni nyumba tatu ikiwamo moja ya ghorofa anayoishi aliyekuwa Mbunge wa Viti maalumu (CCM), Shally Raymond, nyumba nyingine mbili na magari zitakazouzwa kwa njia ya zabuni.TCCCo inamilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa Kilimanjaro (KNCU) chenye hisa 54, Chama cha Wamiliki Mashamba Makubwa ya Kahawa (TCGA) chenye hisa ya asilimia 36 na vyama vingine vinne vyenye hisa asilimia10.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...