Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Hussein Kattanga akizungumza na wakazi wa Kata ya Kindimba Wilayani Mbinga. Katibu Mkuu alipata fursa ya kukagua Mradi wa umeme unaozalisha KiloWatt 1.5 za umeme kijijini hapo. Hata hivyo kutokana na umeme huo kutumika chini ya kiwango Katibu Mkuu alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga kuhakikisha nguzo 60 zinapatikana ili utekelezaji wa kusambaza umeme kwa taasisi na kaya zilizo karibu na mradi wa umeme unakamilika.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Hussein Kattanga akipata maelezo ya ujenzi wa Mifereji ya maji katika Kingo za barabara za Mji mdogo wa Mbinga kutoka kwa Mhandisi wa Halmashauri hiyo bwana Emanuel Mfinanga .Bwana Kattanga aliitaka Halmashauri kuangalia uwezekano wa matumizi ya umeme wa jua katika matumizi ya taa za barabarani.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Hussein Kattanga akikagua ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Wilaya ya Mbinga. Katibu Mkuu aliiagiza Halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa kuongeza sehemu ya kukaa wananchi wakati wakifuatilia uendeshaji wa Vikao vya Baraza la Madiwani.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Hussein Kattanga akisalimiana na Wakazi wa Kijiji cha Tukuzi Wilayani Mbinga. Katika kijiji hicho Katibu Mkuu alipata fursa ya kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa Ofisi ya Mkurabita.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Hussein Kattanga akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kindimba, mara baada ya kukagua miradi ya Maendeleo katika Kata hiyo. Mara baada ya kutembelea Shule hiyo, Katibu Mkuu aliitaka Halmashauri iandae mpango wa kujenga chumba cha maktaba na bweni la wasichana ili faida za kuwa na umeme ziweze kuonekana na sekondari iweze kuwa mfano kwa shule nyingine za Wilayani, Mkoa na taifa kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...