The Strokers, hili lilikuwa kundi jingine la wanamuziki wa Upanga. The Strokers lilikuwa na awamu mbili, ya kwanza ilikuwa na wanamuziki akina Donald Max, David Max, Harry Chopeta, Vincet Chopeta, Pino Makame na Ochiwa na Freddy Lukindo. 
Awamu ya pili ya kundi hili ilikuwa na Sajula Lukindo,Onesmo Kibira,Innocent Galinoma,Ben Galinoma, Denis Pad,Francis Kasambala,Vicent na Harry Chopeta, Ally Mwarabu, Sabri Mmanga na wengineo. 
Pichani ni awamu ya kwanza ya Strokers. Waliosimama, Pino Makame, Freddie Lukindo, David Max. Waliokaa (?),Harry Chopeta, Vincet Chotepa.
Kwa stori za muziki wa Tanzania mtembelee mkongwe John Kitime
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. John Kitime cheki website yako ukifungua ina trojan horse / malware

    ReplyDelete
  2. hawa vijana nikiwaangalia nawaonea wivu kweli kweli. wakati huo wa ujana wao hakuna magonjwa hatari...da

    ReplyDelete
  3. Michuzi asante sana.Hizi picha za zamani huwa nazipenda sana hasa huo ufugaji wa nnywele zao(Afro?),vishati hivyo na visuluari vya kubana.Halafu kulikuwa na viatu virefu sijui vinaitwa 'reizoni'(nadhani raise- on)..Wakati huo kama alivyosema mdau hapo juu..HAKUNA MAGONJWA HATARI KAMA LEO.Halafu uvaaji wao ulikuwa umetulia kweli..ndiyo siku hizi vijana mjini wameanza tena kuvaa namna hii.Inapendeza kweli

    David V

    ReplyDelete
  4. Juzi nilizungumza na ndugu yangu akaniambia walikuwa na ugeni wa Muheshimiwa Makame. Nikamwambia umenikumbusha nduguye. Nikamwambia umenikumbusha mwaka 1977 safari ya kwenda Zenji na ATC na Marehemu Mzee Makame. Ufunguzi wa Uwanja wa Amani, Tatan tracks!

    Sadfa ikanipeleka kukumbuka mtaa wa Magore, Upanga Jeshini, Ubalozi wa Paksitan, Kwa kina nanihii....., halafu kwa kina nanihii...., halafu kwa kina nanihiii..., halafu kwa kwa kina Makame, halafu Duka la Ushirika halafu unaendelee weeee mpaka uchochoro wa Palm Beach! Halafu unavuka barabara kama unataka kwenda Sea View Hotel kucheza disco la Sansui au unapinda kushoto kama unataka kwenda Italian Club/Selendar Bridge Club ya sasa kuburudika na wana Strokers, it is up to you. Damned it...!

    ReplyDelete
  5. Hii mwakitime.blogspot.com imekufa. John Kitime sasa anaendesha wanamuzikiwatanzania.blogspot.com, ambayo hata hivyo inasuasua vibaya sana kwani inaweza kukaa hata miezi miwili bila kuwa na post mpya.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli mwakitime.blogspot.com imekuwa ni njia tu ya kuelekeza blog mpya ya www.wanamuzikiwatnzania.blogspot.com..... karibuni kusuasua kulitokana na kazi ya matayarisho ya onyesho la wanamuziki wenye umri zaidi ya miaka 50. shughuli inaendlea

    ReplyDelete
  7. Duh, Anko Ankal uwe unaweka na miaka basi (19xx - 19xx)ili tukumbukie vema...sio unatoa majina tu!

    Unajua miaka fulani wengine tulikuwa hajatokea duniani!
    Mpenzi wa Xilipendwa-UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...