Moja ya kontena lenye mitambo ya Aggreco likiwasili leo mchana ubungo jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Mahusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Badra Masoud, akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye mitambo ya kufua umeme,  Ubungo jijini Dar es Salaam. Badra alisema kuwa mgao wa umeme utakoma kufikia mwezi Disemba mwaka huu. Akielezea mikakati mbali mbali ambayo TANESCO imefanya ni alisema kuwa ni pamoja na kukodisha mitambo yenye uwezo w kuzalisha Megawati 100, kutoka Kampuni ya Aggreco ya Mombasa, Kenya.

Mitambo iliyowasili leo na kazi ya kuifunga itatarajiwa kuanza hivi karibuni. Akielezea zaidi kuhusu ujio wa mitambo hiyo ya Aggreco, Badra alisema kuwa hii ilikuwa ahadi ya Waziri  wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alipokuwa akiwasilisha bajei ya wizara yake Bungeni hivi karibuni. Mipango mingine ya kumaliza mgao wa umeme ifikapo Disemba mwaka huu ni pamoja na kutumia mitambo ya Symbion yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 112, na mitambo ya Jacobsen inayoendelea kufungwa hatua inayoipa Tanesco uhakika wa kumaliza kero ya mgao wa umeme mwezi Disemba mwaka huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hapa ndipo Tanesco wanaponifurahishaga...Hivi shida ya nchi ni Mitambo ya kufua umemeeee? au ni vyanzo vya nishati..mfano maji, gesi, mafuta na nishati nyinginezo???? Hebu Tanesco mtupe njia mbadala(Alternatives)zote, upatikanaji wa nishati pia ni muhimu, sio inafikia mahali mnasema eti mnazima hiyo mitambo halafu fedha ya kuazima mitambo mnaendelea kuwalipa wenye mitambo. Acheni tu kutoa majibu yasio na solution huko mbeleni. Rais alihojiwa na BBC kuhusu upatikanaji wa Umeme, akajibu "Tanzania haina uwezo wa kufanya Mvua inyeshe"...hivi ni issue ya mvua au ni issue ya mipango mibovu na isiyo endelevu???....Hebu acheni kutufumba na viji-mitambo vyenu vya kukodi hapa! Mnaboa sana!

    ReplyDelete
  2. Yale yale mliyokuwa mnasema kipindi kile gesi ya Songo songo ilipoanza kuzalishwa, na bado mnasema hivyo hivyo.. Tunajua pasipokuwa na mgao vibosile wengi watakufa njaa.

    ReplyDelete
  3. Wakwanza umenena CHANGA LA MACHO

    ReplyDelete
  4. jamani mimi ndio sielewi au
    tatizo la umeme lilikua kwasababu ya vyanzo vya nishati kama maji kupungua sasa kama maji yamepungua na Tanzania hatuwezi tengeneza mvua kama Raisi alivyosema iyo mitambo inakodishwa ili ifue umeme kutoka vyanzo gani au mimi ndio sielewi jamani?
    au ndio yale yale ya viini macho kukodisha mitambo mradi wa watu flani wanapata kula kwao kama ilivyokua kwamitambo mingine
    mmhhh Tanzania kazi ipo

    ReplyDelete
  5. Nauliza hivi ,hili tatizo la umeme hapo disember likimalizika litadumu kwa muda gani ? Au baada ya miezi 6 mgao mpya tena wa umeme ? Tunafahamu kuwa kila mwaka au baadaya miaka 2 matatizo haya huwa yanajirudia kila mara.

    Michuzi tunakuomba utupatie habari kamili juu ya tatizo la umeme kumalizwa ni la muda gani ? Tumechoshwa kuburuzwa na hawa Tanesco. Kamavipi tujiandae na mitambo yetu wenyewe bila ya kutegemea mitambo ya tanesco ambao umekuwa kero toka kupata uhuru.

    ReplyDelete
  6. Kwa nini mitambo ikodishwe? Tanesco haina uwezo wa kununua mitambo yake yenyewe?

    ReplyDelete
  7. Hii inaitwa majoring on minors au danganya toto. Nadhani watanzania hatuhitaji tena hotuba au press conference, Tanesco na au 'mkubwa' yeyote wasizungumzie ufumbuzi wa umeme utatokea lini... tunataka kuuona ufumbuzi bila maneno mengi tumechoka na uongo wa hawa jamaa wakubwa kwa wadogo. toeni tu ufumbuzi bila maneno.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...