Waziri wa maliasili na Utalii Mhe. Ezekiel Maige akiwasilisha Bungeni bajeti ya wizara 
Wabunge wakimpongeza Waziri wa Maliasili na Utalii(katikati)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Wiliam Lukuvi akibadilishana mawazo na baadhi ya Wabunge Dodoma leo.
Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai-Chadema Mhe. Freeman Mbowe akijadili jambo na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Mathias Chikawe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Mhe. Stephen Wasira akimpongeza Mbunge wa Chadema Mhe.Regia Mtema kwa ujasiri wake wa kuliomba Bunge radhi baada ya kutoa matamshi yaliyoashiria ubaguzi wa rangi.Picha na Prosper Minja-Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani nchi hii duh! Haya tunasikia wanyama wanauzwa, wanakwea pipa bila Watanzania kustukia mchezo, vigogo wachache tu wanajua, ndo wanakuja na siri bungeni. Kweli Tz tumelala usingizi. Hivi toka muanze kuiibia nchi bado tu hamjafikiri kizazi chenu kijacho kitafaidi nini? Nchi yetu inahitaji viongozi makini wasiokubali kupokea vicenti kutoka kwa watu wanyonyaji. Sasa hapo Mhe. anapongezwa kwa kuwasilisha bajeti, utadhani anapongezwa kwa kumaliza mtihani, ili akifika home alale sasa. Yaani viongozi wa nchi hii hivi hamjui kuwa mnajiibia wenyewe? Au ndo mnaiibia nchi ili mkaishi mahali pengine? Hivi hamuwazi watoto wenu na wajukuu zenu watarithi nini? Wenzenu tunaumia mioyo sana tunaposikia nchi maliasili zake zinauzwa na wachache! Hebu rudisheni hao wanyama urithi wetu. Hivi mmesikia wapi za wazungu wanauza mali zao? Ni nchi za Afrika tu ndo zinafanya hivyo. Kwa tathmini ya kawaida Tanzania inaweza kulisha nchi zote za Afrika Mashariki pamoja na pembe ya Afrika kwa miaka 5 kama rasilimali zake zitatumika vizuri na uzalishaji utakuwa makini. Badilikeni Bwana ninyi viongozi wetu acheni ubinafsi!

    ReplyDelete
  2. naungana mkono kabisa na mheshimiwa mchangiaji wa kwanza hapo juu hawa viongozi tatizo ni malimbukeni na kukosa kujiamini na uzalendo wakiona rangi nyeupe tu basi wanawaona miungu watu kila watakachoambiwa wao ni sawa mzee

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu umeongea kitu cha maana ,its only happen in BONGOLALA ,maliasili zinauzwa kiholela hata raia hawasemi kitu,tunajua viongozi hawasemi maana wote ni wachafu,kila mmoja anaiba kwa staili yake hivyo mwizi hawezi kumtaja mwizi mwemzake.
    Yaani nchi ni kama kichwa cha mwendawazimu,wananchi wananyanyasika kila leo,hakuna ubinadamu wala huruma watu ni wabinafsi kupita kiasi.Rushwa inaanzia kwenye ngazi za chini sana kama kwa mjumbe wa nyumbakumikumi na katibu kata.
    Hivi ustaarabu upo wapi jamani,tunaomba viongozi wenye sifa za uongozi na elimu ya uongozi na sio kupeana madaraka tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...