Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky akiimba sambamba na Mpiga Bass wake, Hoseah Mgoati . Kuhudu mengi ya vijana hawa wakalai kabisa wa Extra level watembelee kwa ku-BOFYA HAPA
Na Michael Machellah
BENDI ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo Next Level wanatarajia kuwasha moto ndani ya Meeda katika sherehe za Idd Mosi kwa wapenzi na mashabiki wa Sinza Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bendi hiyo, Kamarade Ally Chocky, amesema baada ya kuzikonga nyoyo za wakazi wa Sinza Idd pili watahamia Gongo la Mboto katika Ukumbi wa Wenge ambako wanatarajia kufanya kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa wapenzi na mashabiki wa Muziki wa Dansi.
Alisema Chocky wakiwa katika maandalizi hayo pia Bendi iko msituni katika kurekodi Video ikiandaa albam amabyo mpaka sasa bado hawajaipatia jina.
‘Wapenzi na mashabiki wa Bendi ya Exta Bongo kaeni mkao wa kupata burudani safi na nzuri ambayo hamjawahi kuipata katika kipindi chote kuanzia sasa kutoka kwa vijana mahili wa Kitanzania ambao wanaweza kujisimamia wenyewe na kujiongoza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...