Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwenye kituo cha Mafuta cha GBP pale sinza Mapambano kutokana na vituo vingine vya mafuta kutofanya biashara hiyo kwa kugomea punguzo la bei lililopangwa na Serikali hivi karibuni.Kituo hiki ndicho kituo pekee kilichokuwa kikiuza mafuta kwa leo baada ya vituo kama vya BigBon TSN kuishiwa mafuta kutokana na uwingi wa watu wanaohitaji matuta kwa matumizi mbalimbali.hali hii imepelekea msongamano mkubwa wa magari katika barabara ya sinza mpaka kufikia kufungana na kushindwa kutembea kwa magari kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Ni siku chache tu zimepita tangia Serikali itangaze kuwa imekaa na wauzaji wa mafuta na kusema imemalizana nayo na hakutakuwa na mgomo tena,lakini cha ajabu tangu siku ile hadi hii leo bado mambo ni magumu kama hivi inavyoonekana hapa.
Mmoja wa Waendesha pikipiki maarufu kama Boda Boda ambaye alifanikiwa kupata mafuta baada ya mshike mshike ya nguvu akijiandaa kupakia mafuta hayo kwenye usafiri wake tayari kwa matumizi ya bajeti kama alivyokuwa akiongea mwenyewe pindi mwenzie huyo alieshika vidumu vitupu alipoomba kuuziwa dumu moja hata kwa bei ya juu.
Hakuna uchakachuzi wa foleni hapa,maana kila mtu alikuwa makini katika hilo.
Jamaa wa Boda boda akimimina mafuta aliyouziwa na mwenzake.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika barabara ya Sinza wakati magari hayo yakiingia kwenye kituo cha mafuta cha GBP.
Ni foleni mtindo mmoja.
"Aise"Hii kali...bado siamini ninachokiona hapo picha ya mwisho chini.Poleni wana SINZA.Serikali inawaendekeza hawa wenye vituo vya Mafuta..Wana viburi...wana dharau..nk.FUNGA LESENI ZAO MARA MOJA kwa wale wanaokataa kutii amri zake halali.
ReplyDeleteDavid V
Bongo sasa hapafai. Maji, Umeme, Mafuta zote shida sasa. Foleni sijui zitaisha lini. Hivi wadau mmecheki zile sign za one way katikati ya jiji? Hivi zitaongeza au kupunguza foleni?
ReplyDeleteMnaamini kuwa vituo vya mafuta vinamilikiwa na vio-ngozi (wabu-nge na mawa-ziri)?Maana sijasikia sheria kuchukua mkono wake,wenyewe wanawekewa mafuta ya bure na siri-kali na wananchi wao wanateseka kama tuonavyo kwenye picha ,halafu eti kuna uhuru na demokrasia.
ReplyDeleteHivi usalama wa binadamu upo wapi hapo?je kama ukitokea moto kutokana na mtu kuvuta sigara itakuwaje?
ReplyDeleteTuombeni mungu na haya maisha, utafikiri kama tumekosa radhi za mungu, tuingie misikitini na makanisani tuombe jamani, nahisi hizi ni adhabu za dunia tunazipata kabla hatujafa.
Maji,umeme,vyakula bei juu,uuzaji kiholela wa ardhi,uuzaji wa madini na maliasili kiholela,madawati hakuna ni mawe kwa kwenda mbele,mafuta ndio hayo,nk nk.
SASA ITATOKEA HATARI YA KUFA WATU ....KWANI WATU WATAWEKA PETROL NDANI YA MAJUMBA, SERIKALI ANGALIENI VIZURI HII ITAGHARIMU WATU MAISHA YAO.....
ReplyDeletehapo sasa, eti ni nchi iliyopata uhuru 50yrs ago. Yaani kuna maudhi Tz, na serikali iko kimya. Kikwete baba upo wapi? iko wapi ile tabasamu lako la kuomba kura, tunakulilia please sema jambo kwa wananchi waliokata tamaa na kuchoka kwa maisha. Hivi vyote umeme,maji mafuta ni vitu muhimu sana ktk maisha ya kila siku. Please amueni sasa kimoja kieleweke. Nchi zingine zinakuangalia kikwete maana watoto wako hawa ni wapole nadhani ingelikuwa kenya ungesikia vifo tayari. PLease heshimu huu utulivu wa nchi yetu. Funga hizi leseni za hawa wafanya biashara tuambie kinachoendelea tanesco na idara ya maji. Mhhhhh ni kweli mwenye shibe aijui njaa.
ReplyDeleteHivi hawa ni EWURA au HEWARA. Inakuwaje kituo kinadanganya kuwa hakina mafuta na wao wanakubali badala ya kufunua hayo mashimo yao na kuchokonoa kuhakikisha. Wananchi inabidi tuandamane ili uuzwaji wa mafuta uwe nationalized. Nchi kama za latin amerika hawakubali upuuzi huu. Dawa ni kutaifisha tu kwa manufaa ya uma
ReplyDeleteserikali iko holiday.. puuu! nchi ya ajabu sana kurudi huko itakuwa ngumu sana! haya ni maisha ya machungu kwa kila mlala hoi. poleni sana ndugu zetu!
ReplyDeleteHivi jamani sisi Watanzania upole wetu utakuwa mpaka lini??uvumilivu wetu naona sasa unafikia kikomo,kama serikali imeshindwa kuwalazimisha hawa makabaila wa mafuta kuuza mafuta basi nguvu ya uma ifanye kazi yake.Jamani watanzania huu upole unatufikisha pabaya,haki huwa haiji hivi hivi tu.Rai yangu kwa watanzania wote hasa wa jijini Dar es Salaam tuanze kampeni usiku huu wa kuchoma moto vituo vyote vya mafuta vilivo goma kuuza mafuata. Hicho ndio cha kufanya kwa sasa manake serikali imeshindwa kufanya kazi.
ReplyDeleteTutatia moto vituo vyote vya mafuta vilivogoma kuanzia leo usiku.
Mdau mwenye machungu na mstakabali wa bongolandi
natamani hawa masera wanaochoma moto baishara za watu hapa london waamie tz maana hawa wenye vituo ni wapuuzi na wenye haki ya kuchomewa moto na kukosa baishara kwa mwka mzima au miaka,serikali walisema watafungia mtu mbona hata wa mfano hayupo?
ReplyDeleteBaba Dr. Slaa tia neno hapo, Mbowe, Zitto, Mnyika, mko wapi? au na nyinyi mna share zenu kwenye vituo vya mafuta, kimyaaaaaaaaa, lo salaleeeeee!! Mungu epusha hili balaa Tanzania. Hivi hii nchi inaelekea wapi? Yaani mnaonea Watanzania walivyo wapole eee?
ReplyDeleteBongo hiyooo,maskini na matajiri wote wanataabika tu,Ustaadhi Michuzi hebu tueleze bei ya wese ulipokuwa marekani na pia kama kulikwa na mgao.
ReplyDeleteKwa kweli hali hii inatisha. unatoka kwenye tatizo moja kwenda jingine. matatizo tunayoyalilia sisi Bongo ndio hayo ambayo wenzetu wa Israel wameshindwa kuyavumilia (kupanda kwa gharama za maisha hasa kwa watu wa kati)imebidi wajenge mahema mijini kuonesha masikitiko yao kwa serikali kutotaka kusikiliza haja na matatizo yao.
ReplyDeleteWatanzanie tuamke,serikali iko likizo inakula kuku.Tuingie barabarani tufanye kama walivyofanya wenzetu waisrael. Tunaweza waadhibu wenye jeuri (wamiliki wa vituo vya mafuta) kwa kuiga mfano wa weusi UK wanaochoma moto mali, nasi tuchome vituo vyao vya mafuta.
Tuwape notice ya masaa 24 tu hao wamiliki ndio wasikie jeuri yao. na bima hakuna compasation ya ujinga ktk hilo.
mdau Ughaibuni.
Siku moja nilifata mafuta ya kajenereta kangu,kwenye kituo cha mafuta,mdada wa pale shell akanijia juu na kusema Ewura wamekataza kubeba mafuta kwenye vidumu,nami nikaja juu kwa kumweleza jenereta tutakuwa tunazing'oa na kuzibeba kuja nazo kujaza mafuta? nikawa tayari kununua kesi kama wangetokea.Swali nauliza vipi kama EWURA watasimamia hako kasheria kakutobeba vidumu na hali ilivyo sasa,je patakarika Dar?hahaha sipati picha ,hebu wadau nisaidieni hili maana mie nilikuja juu kweli wakati jenereta ilikuwa nyumbani,sasa fikiria gari imezima hafu mtu anakukataza kubeba kidumu.
ReplyDelete