Wakazi wa Tabata Segerea na maeneo ya jirani na hapo wakisogeza vidumu katika foleni ya kupata huduma ya mafuta kwenye kituo cha Lake Oil kilichopo maeneo ya Tabata Sanene mapema mara baada ya Serikali kutoa tamko la kuvitaka vituo vyote vya mafuta vianze kutoa huduma hiyo haraka iwezekanavyo japo bado kuna baadhi ya vituo vinaendelea kukaidi amri hiyo ya Serikali.
 Mtoa huduka katika kituo cha Mafuta cha Lake Oil kilichopo Tabata Sanene akiendelea kutoa huduma hiyo mara baada ya kupokea amri kutoka kwa bosi wake kwamba aanze kupiga bei wese lililopo kwenye stoku.
 "Eehh... sasa Mafuta tumepata,ila tutaondokaje hapa na wakati tairi halipo??" hivi ndivyo walivyokuwa wakizungumza hawa jamaa ambao walisotea kupata mafuta huku tairi la gari lao likiwa kwa fundi pancha.
 Hapa ni tafrani mpaka msaada wa Askari Polisi huyu aliamua kuingilia kati na kuwataka watu wote kufuata taratibu iliyokuwa imepangwa kituoni hapo.
 Foleni ya Magari na watu wote wakihitaji mafuta.
 Hivi ndivyo mambo yalivyo hivi sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...