Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, baada ya kuwasili katika viwanja vya maghorofa 30 ya Kambi ya Polisi Barabara ya Kilwa kwa ajili ya kuyazindua rasmi leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Maghorofa 30 ya Kambi ya Polisi yaliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Agost 16. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha (kulia) ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa hotuba yake wakati wa kuzindua Maghorofa 30 ya Kambi ya Polisi yaliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo.


KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sijui Polisi wana matatizo au ugonjwa gani!? Yape muda kidogo tu hayo maghorofa utaona jinsi yatakavyochafuliwa na kuchakaa.

    Nilipita pale Mikocheni karibu na Arcade kwenye nyumba wanazoishi maofisa wa Polisi. Yaani ukiziona zile nyumba na mazingira yake zilivochakaa na kuchafuka huwezi kuamini kwamba Polisi walihamia kwenye nyumba zile miaka '80. Tabia hii ya Polisi wa Tanzania kuishi katika mazingira machafu na yaliyochakaa ipo popote kwenye makazi ya Polisi Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Nyumba za madakitari,manasi na walimu (key workers) ziko wapi ?

    ReplyDelete
  3. Hongera kiduchu kwa serikali - 2 out of 10 kwa sababu kazi ndo kwanza inaanza! Kama tunataka taifa lenye kufuata sheria bila kushurutishwa ni lazima law enforcers wawe objectively independent, hardworking, ethical na comfortable (they deserve a good life jamani, hata kwa kiwango chetu cha madafu!) Hizi estate ziwe walau kila mkoa (then later kila wilaya, somebody pinch me pse!). Makazi ya polisi (na wanajeshi) ni aibu ya kitaifa, sometimes hata taasisi hii ikiwa kinara wa rushwa kama baadhi ya tafiti zinavyoeleza tunaona aibu kuiwajibisha, tutaanzia wapi? Hivi kweli mtu alinde mabilioni benki na kusindikiza mijihela kibao halafu anashindia viepe na maji ya viroba? Au amwagwe na mibasi mikubwa ile akeshe kwenye baridi kuwalinda walamaishabora kwenye mihekalu huko uptown huku big a$$ 4x4s na migari mingine ya thamani ikitoka na kuingia getini? Big Bosses endeleeni kushikia bango ishu ya kuboresha maisha ya 'manjagu', otherwise hakutakuwa na mahusiano mazuri na raia coz jamaa watachoka uvumilivu, watakua wanalipua tu kazi yao bila ufanisi wala uelewa wa sheria na haki za binadamu. Sijui Kamanda Mwema kashikia bango hii ishu na yeye ajenge legacy yake? Either way, good job kwa 'sirikali'.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...