Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA ) Mama Salma Kikwete akisoma nakala ya RAPID WOMEN Model ambayo ni kitendea kazi cha utetezi wa uzazi wa mpango na afya zinazomlenga mwanamke, matumizi ya kielelezo hicho yanalenga zaidi wanawake viongozi katika kuhamasisha jamii. Muundo huo wa kitendea kazi uliwasilishwa na Dr. Sara Clark (hayupo pichani) ambaye ni Makamu Rais na Mkurugenzi wa Kampuni ya Futures Group International leo katika ofisi za WAMA zilizopo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dr. Sara Clark (kushoto) ambaye ni Makamu Rais na Mkurugenzi wa Kampuni ya Futures Group International akimuonyesha Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA ) Mama Salma Kikwete (kulia) mfuko wa kuwekea vitu mbalimbali ambayo inatumika kama matangazo inayotengenezwa na kampuni hiyo wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuwasilisha muundo wa kitendea kazi cha utetezi wa uzazi wa mpango na afya zinazomlenga mwanamke.
Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) (katikati) Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Dr. Sara Clark (kushoto) ambaye ni Makamu Rais na Mkurugenzi wa Kampuni ya Futures Group International na Millicent Obayo ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa kampuni hiyo wakati walipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuwasilisha muundo wa kitendea kazi cha utetezi wa uzazi wa mpango na afya zinazomlenga mwanamke.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...