Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete (kulia) akiwakabidhi zawadi baadhi ya walimu wanafunzi saba kutoka Tawi la Chuo cha Ualimu St. Augustine tawi la Mtwara leo walipokwenda kumuaga ofisini kwake baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu kwa vitendo katika shule ya mfano ya watoto yatima WAMA-NAKAYAMA Mkoa wa Pwani,katikati ni Mwalimu mwanafunzi Kaiza Magoa na (kushoto) Kiongozi wao Victoria John.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete (kulia) akiongea na walimu wanafunzi kutoka chuo cha Ualimu St. Augustine tawi la Mtwara waliomaliza mafunzo kwa vitendo katika shule ya mfano ya watoto yatima WAMA -NAKAYAMA iliopo chini ya Taasisi ya WAMA, huko Rufiji mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (mwenye baibu) akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wanafunzi kutoka chuo cha ualimu ST. Augustine, tawi la Mtwara waliokwenda kumuaga ofisini kwake leo baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu kwa vitendo kwenye shule ya mfano ya watoto yatima WAMA-NAKAYAMA inayofadhiliwa na Taasisi ya WAMA huko Rufiji mkoa wa Pwani.Mstari wa nyuma alievaa T-Shirt ya mistari ni Katibu wa WAMA, Daud Nasib (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...