URBAN PULSE CREATIVE member Frank Eyembe wakishirikiana na Freddy Macha (shoto) walipata fursa ya  kupitia mji wa Tottenham uliopo katika jiji la london ili kujionea kwa macho hali ilivyo kwa sasa. Program hii imerekodiwa kwa kutumia Simu ya mkononi. Karibuni katika safari hii...
Asanteni.
URBAN PULSE CREATIVE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ankal Duu mji wa Tottenham?

    ReplyDelete
  2. UK ni nchi ambayo ina sheria nzuri sana lakini huwa kwa wenyewe. Mtu wa rangi huwa taabu sana kutumiwa hizo sheria kwao. Ndio maana wameongeza sheria nyengine kwa watu wakuja kuwa akifanya kosa la kufungwa basi atatumikia muda jela akimaliza tu atarejeshwa kwao. Mtu wa rangi mpaka atumie nguvu ndio afikiriwe kutumiwa sheria.

    ReplyDelete
  3. Bwana Macha naomba nikukosoe katika maelezo yako,kwanza hizo riots the main reason behind it ni deficiency economic empowerment for minority especially those carribeans blacks,dont compare other immigrants with them,those are like natives british the same situations of Blacks in USA,british government ignores them for a long time,no any social project to let them effective intergrate in the community,people are economicaly and socialy hopeless,kwa hiyo hizi vurugu it was part of their furious expression of their feelings,in psychiatry we call it "acting out".
    Na pia hakukuwa na uhusiano wowote kunasibisha Gays with the police tolerance against protesters,these are the world wide human right,its part of freedom of speech and expression,you will never find any western countries police to act aggressively against protesters,kwa hiyo labor sidhani kama wamehusika na hiyo sheria.
    Thanks
    Mdau USA

    ReplyDelete
  4. Wewe una mtazamo tofauti na ukweli,watu waliofanya fujo wanadai haki ambazo in normal means muda mrefu hazisikilizwi.Hata ukiona mijadala na maoni ya wanasiasa wa Uingereza wanakubali na kwa faida ya wote,usichukulie mawazo ya watu waliokuja kuupanchi apewe nyumba ya bure kazi yake iwe kuzaa tu walishwe bure bure hapana hiyo.Kwa watu waliotoka Zanzibar,na wengine kuuza hata nyumba aombe ukimbizi fake ili alishwe na serikali ni sawa,lakini kwa mtu anaetaka heshima ni tofauti,lazima uwe na mtazamo wa fikra za kisasa.Ni aibu ubanwe ili uwe unapewa wlfare unajiabisha kama binadamu.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa USA napingana na wewe na kama uko huko USA ni bora ubadili fikra yako usiingie kwenye band wagon ya mawazo hasi. Message ya huyu bwana iko very clear na mamuunga mkono kwa 100%. Hata kama huko nyuma kulikuwa na unyanyasaji wa wausi halisi, sasa wabadilike kimawazo na wapambane kimaisha sababu wageni wanaokuja ambao wengine ni weusi kama wao wanapambana na wanafanikiwa kuliko wao!! Kwa maneno mengine si kweli kwamba weusi (halisi wa UK na US) hawawezi kufanikiwa sababu waghana, wanigeria, wazimbabwe, wakenya nk ambao hata kiingereza chao ni cha kudodosa wanafanikiwa. Nimeona nitoe hii comment sababu hili tatizo la fikra potofu za weusi asili wa US na UK linasababisha wawe na HATE kwa weusi wenzao wanaohamia sasa na wahamiaji kwa ujumla. Hawataki kujishughulisha na wakikuona wewe mgeni unafanikiwa wanaku hate!! Wengi wanachagua kazi, wageni wanakuja USA na UK wanafanya hizi hizo kazi wanazozikataa, wanasomesha watoto wao hadi University na wanaweza kuleta ndugu hata bibi zao wao wamebaki wanalalama!! Hao vijana uliowaona wanaandamana kuna kijana mwingine wa umri wao kwa sasa yuko Nigeria, Ghana au Kenya lakini amini usiamini kijana huyo siku zijazo atahamia UK atafanikiwa kuliko hao waliokuwa wanaandamana na watabaki kuendelea kulalama tu. Nakubaliana kuna ubaguzi ndio lakini mbona wageni wanafanikiwa? Kama mtu unajua mfumo huwezi kuubadili ina maana ni busara wewe ulalame tu wakati wenzako wanakuja wageni na wana win kwenye mfumo huo huo? Jibu ni hapana.
    Kuhusu maoni yake ya gays alikuwa anatoa mfano tu wa sheria ya haki za binadamu inavyosaidia makundi mengine ambayo wenye nchi zao wananyanyaswa. Clip imenipa picha ya kilichotokea hasa kuzingatia mtu anahojiwa na kuendesha gari...

    ReplyDelete
  6. kwa kujua nini kilisababisha fujo tembelea bbc iplayer young voter question time,hapo vijana na ex gang wanaongea,macha ujajiandaa kwa kifupi na hizo fikra zako za fujo.

    ReplyDelete
  7. I'm shocked to view This biased Video; Yaani Wanaongelea Mabaya ya Watu Weusi Asili Uingereza Wanawasema Vibaya.

    Tatizo ni Social and Economic Dev. of Black People from Britain; wamenyang'anywa haki zao hakuna kazi, malazi, na Chakula wanaishi kwenye Government houses no development na social services kwa watu ambao hawana pesa zinaondolewa na hii Serikali ya Conservative...

    Yaani Watanzania hawa wawili ni Aibu, Wamesahau Siasa ya Ujamaa jinsi inaovyoongelea Ubepari?

    Ni Aibu Kweli na Inasikitisha

    Tiron, New York

    ReplyDelete
  8. Upo UK kweli hata ndevu hujanyoa au ndo box lilikuwa limekubana.
    You should to be smart compared with wasomi

    ReplyDelete
  9. Kwanza jamaa kaniacha hoi alipouliza ingekuwaje kama "Mheshimiwa Rais wa hapa" angekuwa na FFU kama wa kwetu. Dah! Uingereza ina Rais? Video iko very shallow kwa kweli. Ni vigumu ku learn chochote kwenye hiyo video. Pili jamani tuwe tunajitahidi kuwa a bit professional katika kuchukua video kwa ajili ya media hata kama ni social media. Mtu unachukua video ukiwa kwenye gari? Kwa nini msingeshuka kwenye gari na kutembelea sehemu husika na kuchukua hiyo video? Hii biashara ya mahojiano kwenye gari is becoming too much embarrassing kwa wabongo. Hatutaki kujiumiza.

    ReplyDelete
  10. Nyie watu wa US tunawajua kwa ubishi wenu, achoongea Macha ni kweli na hata wengi walioko uk watamuunga mkono. Sioni wapi Macha alikosea isitoshe alikua anaendesha na mnavyojua trafic kwenye hizi nchi za wenzetu. Macha tunashukuru sana maana wengi tulikua hatujui kina hasa cha ugovi huo, ulitumia mda wako kujitolea kutujulisha kwa ufasaha. Kilichobaki ni sisi wabongo kujua hizi nchi za watu zinakua na mabadiliko na huenda maisha yakawa magumu sana kwa wahamiaji wanaokimbia kwao kutafuta maisha bora. Inabidi tujipange turudi Bongo na kuijenga nchi yetu kama za wenzetu, na tuacha longolongo zisizokua na maana. Asante sana

    Mdau Helsinki Malmikartano

    ReplyDelete
  11. Huyo mdau anayesema watu wametoka TZ, Nigeria, Kenya wamefanikiwa na kuuliza itakuwaje weusi asili wasifanikiwe? Jibu ni kuwa hao wageni waliofanikiwa ni kuwa tayari wameshafanikiwa tangu makwao. Sasa subiri watoto wao baada ya miaka 20 ijayo je watapata mafanikio kama wazazi wao? Huyo aliyetengeneza hii filamu muulize kwanini anatengeneza filamu hii kwa kushirikiana na wabongo baadae auzie tv za bongo? Kwanini biashara yake ilenge soko la TZ badala ya UK? Kwa taarifa yako mzungu yeyote yule ambaye unamuona hana maendeleo hapa UK basi huyo yeye mwenyewe hataki hayo maendeleo. Mfumo wao wa elimu unamruhusu yeyote yule kusoma "entry qualification" yao kubwa ni umri na uzoefu wa kazi.

    ReplyDelete
  12. (Niliyesema kuhusu waliotoka Nigeria na Ghana) naendelea.....Weusi wa asili hawafanikiwi sababu hawana initiative na wanataka kujilinganisha na weupe kitu ambacho hakiwezekani (REALITY, UNFORTUNATELY!). Kuna wazazi wa kiafrika ninao wafahamu ambao wame instill fikra za kujituma badala ya kulalama na watoto wao wanakwenda mbali ingawa wamezaliwa ughaibuni. Ni problem ya fikra ukiacha mambo mengine systemic. Kijana wa kimarekani anataka acheze basketball, aimbe, nk apate millions within no time na hiyo ndio American Dream yake, akikosa analalama na kupinga system yote. Wakati mwingine aliyetoka Africa anakwenda huko anasoma na kupata kazi, HATA KAMA KAZI ZI NZURI lakini anaishi maisha better kuliko yule anayeota American Dream na kusikiliaza mziki 24/7!! Sisemi kwamba watu wasidai haki zao lakini kudai haki na kulalama kuendane na kujishugulisha vile vile sababu si kweli kwamba hakuna opportunities!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...