Mashindano ya Tennis ya wazi ya CRB Africa Legal yamemalizika kwenye viwanja vya gymkhana huku ikishuhudia vijana kadhaa wakionesha vipaji vikubwa mbele ya kocha kutoka Italia Fabrizio Calderon aliyekuja kuangalia vipaji vya vijana katika mchezo huo.Picha juu ni watoto hao wakionesha vikombe na medali walizotwaa katika mashindano hayo ya aina yake.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo, kocha Fabrizio kutoka Italia amesema ameridhishwa na viwango vya vijana walivyoonesha katika michuano hiyo ya CRB na hakusita kusema kuwa vipaji vipo Tanzania kwa mchezo huo.
Kocha Fabrizio Calderon akiwa na mshindi wa pili wa mashindano hayo kwa watoto wa chini ya miaka 10 Shadya Maulid Kitenge mara baada ya kumkabidhi kikombe na medali kwa ushindi wake wa pili wa mashindano hayo.


Na mshindi wa kwanza chini ya miaka 10 ni mtoto wa nani?
ReplyDelete