Mbunge mteule kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mussa Khamis Silima, alipata ajali juzi katika eneo la Nzuguni, Dodoma, ambapo mkewe, Mwanaheri fahari, alifariki dunia na yeye na dereva wake kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospital ya Muhimbili kwa matibabu zaidi
Dereva Chezani Sebunga aliyekuwa akiendesha gari la Mbunge, Mussa Khamis Silima na kupata ajali eneo la Nzuguni, Dodoma , akiwa katika machela akiingizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo asubuhi, akitokea mkoani Dodoma. Mke wa Mbunge Silima, Mwanaheri Fahari alifariki dunia katika ajali hiyo. Mbunge mteule kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mussa Khamis Silima, ambaye alipata ajali juzi katika eneo la Nzuguni, Dodoma, akiwa katika machela baada ya kushushwa kwenye gari jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, alikoletwa na ndege kutoka Dodoma. Mke wake, Mwanaheri Fahari alifariki na dereva wao Chezani Sebunga alijeruhiwa kwenye ajali hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Mwili wa mke wa Mbunge Mussa Khamis Silima, Hayati Mwanaheri, ukiombewa dua na Wabunge n waombolezaji wengine baada ya kuwasili katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa mjini Dodoma leo kuswaliwa kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa mazishi. Marehemu alifariki Jumapili jioni kwa ajali ya gari katika eneo la Nzuguni, nje kidogo ya mji wa Dodoma
Mwili wa Marehemu ukiingizwa msikitini kuswaliwa kabla ya safari
Gari la mafuta lililohusika katika ajali hiyo ambapo mfanyakazi wake anaonesha mahali ambapo gari dogo lililokuwa na marehemu na mumewe kugonga wakati likitaka kupita
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo akimweleza mbunge wa Mafia, Mh Shah, kilichotokea
Mbunge wa Mafia Mh. Shah akiliangalia gari dogo la Mh. Silima lilivyoharibika baada ya ajali hiyo
Baadhi ya wabunge wakiwa chumba cha maiti cha hospitali ya Dodoma kusubiri kuchukua mwili wa marehemu |
Poleni kwa Msiba. Barabara zinazojengwa hazina std. Ni nyembamba mno
ReplyDeleteWembamba wa barabara si sababu ya msingi ila ni maamuzi sahihi ya madereva
ReplyDeletenimesikia na mh mbunge amefariki mchana huu....pole kwa wanafamilia
ReplyDeleteKuna barabara nyembamba kama UK? Lakini sheria zake zilivyo kali mwenyewe utaendesha kwa adabu. Sheria za kwetu bado sana na watu hawaogopi hiyo adhabu ndogo. Nazungumzia barabara ambazo sio highway. Na vile vile wasingesafiri usiku jamani its too risk kwa sababu ni muda ambao magari makubwa yanaruhusiwa kusafiri. All in all innallillahi wainaillaihi rajiun
ReplyDeleteSHEIKH MICHUZI,
ReplyDeleteHIVI MTU ANAPOKUKABIDHI KITU CHAKE UMUUZIE NADHANI UTAKIUZA KWA BEI ITAKAYOKUWA SAWA AU JUU YA BEI ALIYONUNULIA AU GHARAMA YA KUTENGENZEA. SASA IWEJE SERIKALI IWAKAMATE WATENDAJI WA BP ILIHALI WATENDAJI HAO WALIOMBA RUHUSA KWA SERIKALI IWARUHUSU WATENDAJI WAUZE KWA BEI YA HASARA KAMA EWURA ALIVYOKURUPUKA KUITANGAZA HADI LEO SERIKALI HAIJATOA IDHINI HIYO. NADHANI HAPA PANABIDI MJADALA ILI WATANZANIA WAELEWE UKWELI. JEE SERIKALI ITAWEZA KUJISHTAKI YENYEWE?
kila kitu kinataka sibabu huwo ndio mwisho wa binadamu RIP.
ReplyDeletehuwo ndio mwisho wa binadamu, kila kifo kinataka sibabu RIP
ReplyDelete