Gari ikiovateki katika mwinuko huku gari nyingine ikija kwa mbela katika barabara ielekeayo Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja,Zanzibar mchana wa leo,kitu ambacho ni hatari sana na inaweza sababisha ajali kutokana na uzembe wa namna hii barabarani.
Abiria wakiwa wamening'inia kwenye Gari la abiria maarufu "Chai Maharage" kutokana na gari hilo kupakia abiria zaidi ya uwezo wake.
Gari la abiria likiwa nimepaki katika barabara sehemu ambayo haina kituo cha kupakilia abiria maeneo ya Bububu,Zanzibar mchana wa leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Duh, mara ya mwisho kwenda Z'bar ilikuwa mwaka 2001 tulipanda chai-maharage...yaani bado magari hayo yapo tu? Watalii nao wahszoea kuning'inia Tz bara labda chai maharage ya kwenda shamba!
    Mdau-UK

    ReplyDelete
  2. Inaelekea mpiga picha umebabaishwa na 'photo perspective' kwani huyo 'overtaker' anafanya hivyo baada ya kuruhusiwa na wa mbele yake na bila shaka baada ya kuridhika na hali ya usalama. Angalia hizo indicator zao kama unaelewa maana ya matumizi yake!

    ReplyDelete
  3. AHSANTE KWA TASWIRA ZA BARA NA ZANZIBAR JE WADAU MMUMEONA TOFAUTI YA MUUNGANO HAPO? WENYE SERIKALI HATA ALAMA ZA BARABARANI HAKUNA LAKINI WASIOKUWA NA SERIKALI KUNA MAJUMBA YA WAWEKEZAJI WA KILA AINA,INASIKITISHA SANA HATA ALAMA YA AINA YOYOTE YA BARABARA HAKUNA,USAFIRI NI BAISIKELI TU UNAONGOZA,WAKATI TAASWIRA ZA JUU TUMEKUTA FOLENI YA MAGARI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...