![]() |
| Hayati Mussa Khamis Silima |
Mbunge Mussa Khamis Silima wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar, amefariki dunia.
Akitoa taarifa hiyo Mh. makinda amesema , asubuhi amesema kuwa alitoa taarifa kuhusu ajali ya Mbunge mwenzetu eneo la Nzuguni na kwamba mke wake alifariki papo hapo,
“Na nilisema kwamba dereva wake na Silima walipata majeraha makubwa na wamepelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
“Nimepokea taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa Mheshimiwa Mussa Khamis Silima amefariki dunia muda mfupi uliopita/"Kwa mujibu wa kanuni ya 149 ya Bunge toleo la 2007, naahirisha shughuli za Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi,” alisema na kuomba kukutana na Kamati ya Bunge ya Uongozi kuzungumzia na
kupanga kuhusu msiba huo.
Hayati Silima akiwa na mkewe Mwanaheri dereva, walipata ajali mbaya katika eneo la Nzuguni, Dodoma juzi usiku wakitokea Dar es Salaam baada ya kuhudhuria mazishi ya shemeji yake na kusababisha kifo cha mkewe. Yeye na dereva walijeruhiwa vibaya na kuhamishiwa Muhimbili kitengo cha Mifupa MOI kwa matibabu zaidi.a



Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
ReplyDelete"Verily we belong to Allah, and to Allah we return."
Inna lillaah wa inna illaah rajiun. Mwenyezi Mungu awaweke mahala pema peponi, Amin.
ReplyDeleteDUH POLENI WAFIWA JAMANI CKU HIZI TUNAKUFA JAMANI TUMRUDIE MUNGU TU MANA DUH,MWAKA HUU NI NOMA TUNAENDA ILE MBAYA YAANI.
ReplyDeleteJamani Mungu awaweke mahali pema peponi. Waandishi wa habari mnaporipoti habari za ajali nasisitiza neno hili AJALI MBAYA. Ajali kwa vyovyote itavyokuwa haiwezikuwa kinyume cha ajali mbaya. Ajali zote ni mbaya. Hivyo unavyoripoti ajali ukaitofautisha na ingine kwa kusema ajali hii ni mbaya si sahihi. Nachoshauri mseme tu ajali iliyosababisha kifo, ama majeruhi
ReplyDeleteMwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi. Poleni sana wafiwa sana sana watoto wa marehemu. Jamani hivi watu wangapi watakufa katika hizi ajali mpaka serikali ichukue hatua. Wameshindwa kabisa kuzuia hizi ajali. Hata ukiweka polisi 10,000 barabarani zitatokea tu. Inabidi vile vile muundo wa barabara ubadilishwe, kama vile kuweka overtaking sections (crawler lanes)katika sehemu za milima. Ankal, mimi ni mtaalamu wa mambo haya na ninafanya kazi Uingereza na nitapenda sana kusaidia nchi yetu ili kupunguza janga hili. Hii barabara ya kuelekea Dodoma imetupotezea watu wengi sana, inabidi iangaliwe upya. Kwa hiyo kama kuna contact zozote zile (hata serikalini) ili kufanikisha kazi hii naomba tuwasiliane. Nitakutumia email yangu, jamani imetosha, kama serikali haiwezi kukabiliana na janga hili, watangaze vijana tuingie kazini.
ReplyDeleteNingeshauri barabara ya Moro-dom ifanywe double mara unapoingia dodoma hasa kuanzia pale ihumwa. Ni nyembamba sana hasa maeneo ya Nzuguni wakati magari yanaongezeka Kila siku. Nchi igelikuwa na pesa za kutosha ingefaa highway zote nchini zifanywe double (yaani wanaokwenda watumie barabara yao na wanaorudi watumie ya kwao)huku zikiwa zimetenganishwa na tuta kaikati. Itapunguza ajali kwa kiasi kikubwa. Lakini si vibaya serikali ikaanza kulifikiria hili kama mkakati wa muda mrefu katika kukabiliana na ajali nchini.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu ampe maghfira na ammpe jannah. Amin.
ReplyDeleteInnallillah waina illahi rajiun
ReplyDeleteNamfahamu Marehemu tangu akiwa mwalimu wa Sekondari Zanzibar na hata hivi akiwa bungeni tulikuwa pamoja muda mwingi wakati wa vikao Dodoma, InASIKITISHA LAKINI NDIO MWISHO WA MWANAADAM
seleco
Dereva wake ndio chanzo cha ajali, coz alikuwa ni mzembe according to RPC.Madereva wa bongo bado wanahitaji shule sana mara nyingi decision zao huwa ni mbaya. kabla ya ku-overtake unatakiwa ufanye observation and then uchukue right decision. Nafikiri leseni ya alipewa.Inasikitisha family inapoteza watu kwa uzembe wa mtu mmoja. Inabidi nae afunguliwe shtaka la uzembe mara moja. RIP mbunge wetu
ReplyDeletewewe anony wa 02.32 akili yako UGORO mtupu tumrudie Mungu unafikiri wanaokufa wana dhambi au wanaoshi hawana dhambi? Chunga sana kabla ya kuandika huo UGORO wako.
ReplyDeleteMungu ndie aliyeta na mungu ndie aliyechukua jina la bwana lihumidiwe milele, Poleni sana watoto,ndugu, jamaa na marafiki
Watu wengine akili finyu kama tundu la sindano, hivi unataka ajali isiandikwe ni mbaya wakati imechukua uhai wa watu, stupid, kuna ajali mbaya na isiyokuwa mbaya, isiyokuwa mbaya ni ile gari tu ndo linaumia na inayokuwa mbaya watu wanaumia, kumbuka gari linaa spare mwili hauna. Maskini mlio fiwa poleni sana naamini Mungu anawatia nguvu na soon mtakuwa ok. Tuombee waliobaki zaidi waliokufa hawawezi tena kutubu ndo hivyo wamekufa wamekufa nothing we can do
ReplyDelete