Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowasa akimpokea Mchezaji wa mpira wa kikapu toka nchini Marekani ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya D12 Foundation ya nchini humo,Dwight David Howard wakati alipokuwa akiwasili jimboni humo.
mchezaji wa kikapu wa timu ya Orlando Magic ya nchini Marekani ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya D12 Foundation ya nchini humo,Dwight Howard akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh,90 milioni kwa mkuu wa shule ya sekondari ya Kipok iliyopo wilayani Monduli,Felister Lukumay kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni shuleni hapo jana,katikati anayeshuhudia ni mbunge wa jimbo hilo,Edward Lowasa.
Dwight Howard akiwa na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowassa pamoja na mkewe,Regina Lowassa mara baada ya nyota huyo kutembelea shule ya sekondari ya wasichana ya Kipok iliyopo wilayani Monduli juzi na kutoa msaada wa kiasi cha fedha 90 milioni kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafuzi shuleni hapo.
Dwight Howard akiwa na wadau.
Dwight Howard akiwa na wanafunzi mbalimbali wa  shule ya sekondari ya wasichana ya Kipok iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha wakati alipotembelea shuleni hapo na kumwaga mamilioni ya fedha kusadia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi shuleni hapo.
Mchezaji wa mpira wa kikapu toka nchini Marekani anaechezea timu ya ,Dwight David Howard (katikati) akiwa Mbunge wa jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) wakati mchezaji huyo alipofika jimboni humo kwa kuchangia masuala ya elimu.
Mchezaji wa mpira wa kikapu toka nchini Marekani,Dwight David Howard akiwapungia wakazi wa Monduli. Pata habari zake kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Basketball ni wachezaji watano kila upande (NBA) ila always hili lijamaa likiwa uwanjzni utadhani Magic wana wacheza saba, the usual five plus two additional walio inbuilt kwa mchizi!

    Dah, wengi sana tunatamani Hasheem Thabeet angekuwa anafanya haya. Kaza msuli mwanetu, you still young and you got in your hands a one in a million chance to make it really big! May God give you wisdom, courage, strength and a really 'thick skin' manake haters wako wengi sana na wana-discourage kichizi.

    ReplyDelete
  2. The Best Center in NBA I'm so proud for him touring in Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Mfano kwa Hasheem Thabeet jinsi social responsibility inavyotakiwa kuwa, hata yeye angeweza kuyafanya haya....

    ReplyDelete
  4. Hongera wakazi wa monduli kwa kutembelewa na Super Man-DH,jamaa katoka kwao na kaacha kila kitu kaja bongo na kasaidia shule,viongozi wetu haswa wale wenye VIJISENT hata kuchimba kisima tu kwenye shule hawawezi.
    Tuwe na moyo kama wa hawa jamaa,lakini pia hawa jamaa wanafanya kazi kwa bidii sana,huwezi kuamini, wana mda mdogo sana wa kufanya starehe,
    lakini sisi starehe ndio mbele kuliko majukumu ya taifa.

    ReplyDelete
  5. Kweli kabisa mdau wa kwanza inatusikitisha Thabeet anjinyima nafasi ya kufanya mambo kama haya..

    ReplyDelete
  6. Jamaa kaenda hewani,duh

    ReplyDelete
  7. Msimponde Hasheem bure, ukoo wake tu unatosha kuwafanyia hayo maana wamajjiiii!!

    ReplyDelete
  8. Ni faraja kubwa kwa mtu kuwa hana Asili ya sehemu/mahala fulani na akaweza kijitoa kwa kusaidia kwa hali na mali, mimi binafsi yangu namponeza sana kaka yetu, ila pia iwe changamoto kwa sisi wazawa je tunafanya nini kwa nchi yetu na pia tutafikia hatua ya kuweza kusaidia mahali tusipo na asili napo?

    Mh Lowasa pia nimefurahi kwa wewe kushuhudia swala hili kama mwakilishi wa wananchi naomba iwe pia chachu kwako kuweza kusaidia watu wenye mahitaji.

    MUNGU WABARIKI WOOTE WALIOFANIKISHA HAYA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...