Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na mkewe mama Mwanamema Shein wakisaidia kuchambua karafuu wakati wa ziara ya Pemba wikiendi hii.
Jumla ya Tani mia moja sitini na tano nukta moja nne za Karafuu zenye thamani ya shillingi Billioni mbili millioni mia mbili sabini na sita laki sita hamsini na tano elfu zimenunuliwa katika kipindi kifupui cha Uvunaji wa wa zao hilo Kisiwani Pemba.
Meneja wa ZSTC Pemba Hamad Khamis Hamad amemuelezea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohd Shein hivi leo huko Mkoani Pemba kuwa ZSTC kwa muda mfupi tokea kuanza kununuwa zao hilo katika vituo vyake mbali mbali tayari imefanikiwa kununuwa tani hizo kwa Wakulima waliokwenda kuuza Karafuu zao katika Shirika hilo.
Hamad amesema kuwa Mkoa wa Kaskazini Pemba umeweza kuuza jumla ya Tani kuminatisa nukta nane sawa na shillingi Millioni mia mbili themanini laki saba arobaini na moja elfu mia saba na hamsini.
Kwa upande wa Mkoa wa Kusini Pemba Shirika la ZSTC
limenunuwa jumla ya Tani mia moja na Arobaini na tano nukta mbili sita sawa na shillingi Billioni moja millioni mia tisa na tisini na tano, tisini na moja elfu,elfu tatu mia mbili na hamsini.
Mapema Dk Shein amewashukuru Wananchi na Wakulima wa maeneo mabli mbali ya Pemba kwa kuitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuuza Karafuu zao katika ZSTC.
Amesema nia ya Serikali ni kuimarisha zao hilo kuanzia sasa na ndio maana ikaongeza Bei ya Karafuu kutokana na kupanda kwa Bei katika Soko la Dunia, lakini pia amesema ni kuwasaidia Wananchi wenyewe ili kukabiliana na MAKALI ya maisha.
Dk Shein ameeleza kuwa Serikali imejiandaa kwa kuwapatia MICHE ya Mikarafuu bure katika kipindi kijacho hivyo amewasisitiza Wakulima wenye Mashamba ya Mikarafuu kutayarisha Mashamba yao katika kuyaweka katika hali ya usafi ili waweze kufaidika na MICHE hiyo.
Akizungumzia kuhusu kupanda kwa bei ya vitu, Dk Shein amesema kuwa Serkali imeliona tatizo hilo ambalo sio la Zanzibar pekee, kwani ni la Duniani kote hata hivyo amesema kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itajitahidi katika kipindi kijacho kufufua Kilimo cha Mpunga kwa kuwawezesha Wananchi kwa kuwapatia zana za Kilimo ikiwa ni pamoja na kuwapatia Mbegu za kisasa ya NERIKA kwa lengo la kujitosheleza kwa Chakula.
Katika ziara yake kwa siku ya pili kisiwani Pemba leo Dk Shein alitembelea Kambi za Karafuu Chake Chake, Mtohaliwa na pia Mkanyageni kituo cha ununuzi wa Karafuu.



Yakhe tuketi...
ReplyDelete